Nenda kwa yaliyomo

24: Redemption

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
24: Redemption
MudaToleo la Utangazaji:
d.k. 89
Toleo Lililorefushwa:
102 min.
AinaKupigana/Drama
Imetungwa naHoward Gordon
Imeongozwa naJon Cassar
NyotaKiefer Sutherland
Cherry Jones
Colm Feore
Robert Carlyle
Hakeem Kae-Kazim
Tony Todd
Powers Boothe
Eric Lively
Peter MacNicol
Jon Voight
Kris Lemche
Nchi Marekani
LughaKiingereza
Kituo halisiFox
Tarehe ya kutolewa23 Novemba 2008
Ilitanguliwa na24 (msimu wa 6)
Ikafuatiwa na24 (msimu wa 7)

24: Redemption ni filamu ya televisheni kutoka katika mfululizo wa televisheni wa 24. Ilianza kurushwa kwa mara ya kwanza mnamo tar. 23 Novemba 2008, kupitia kituo cha Fox cha nchini Marekani, na baadaye kutolewa katika DVD mnamo tar. 25 Novemba. Filamu ilitungwa na matayarishaji mtendaji Howard Gordon, na kuongozwa na Jon Cassar. 24: Redemption huchukua nafasi baina ya msimu wa sita na saba, na inaelezewa katika muda wa kawaida baina ya saa 3:00 mchana na 5:00 jioni ya Siku ya Uzinduzi.

Mpango mzima upo katika nchi ya Sangala, nchi ya tamthilia tu ya Afrika, mahali ambapo Jack Bauer (Kiefer Sutherland) anajaribu kujitafutia amani ya nafsi, na kufanya kazi kama mmisionari na Carl Benton (Robert Carlyle), ambaye ndiye aliyejenga shule ya Okavango ya kuwasaidia watoto yatima walioathirika na vita. Jack anatumikia hati ya kuitwa shaurini - kuonekana kabla Baraza la Seneti la Marekani halijaanza kusoma shauri la ukiukwaji wa haki za binadamu, lakini alikataa wito huo. Muda huohuo, asasi kivuli miongoni mwa serikali ya Marekani wanamsaidia Jenerali Juma (Tony Todd) na kikosi chake cha jeshi.

Jina la kazi lilikuwa 24: Exile. Wazo la filamu lilianza tangu Mgomo wa Chama cha Waandishi Marekani wa 2007-2008, ambapo kulikuwa na mchelewesho wa kutolewa kwa msimu wa saba kwa mwaka mmoja, na kuacha nafasi wakati wa mwaka wa 2008. Redemption ilifanana kidogo na Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ya mwaka wa 1994. Sehemu ya utengenezaji wa filamu ya Redemption ilipigwa nje kidogo ya mji wa Cape Town, Afrika Kusini, kwa kuwa watayarishaji waliona-vigumu kuigiza mazingira ya Kiafrika nchini Marekani.

Toleo la DVD la Redemption mara-nyingi huwa na toleo la ziada la filamu. Toleo halisi lilirushwa hewani na kutazamwa na zaidi ya Wamarekani milioni 12, na kupewa tahakiki za hali ya juu, na wengine kusema kwamba filamu kidogo imeitatiza msimu wa sita, vilevile sifa za kuonesha maisha ya kibinaadamu zaidi kwa Bauer. 24: Redemption ilichaguliwa mara moja katika Golden Globe mara tano katika Emmy Awards. Hata hivyo, hakuna hata moja katika hizo kutokea kushinda.

Redemption inaanza na utangulizi mfupi unamwonesha kijana mdogo mmoja anayetekwanyara usiku wa manane, akifunzwa, na kupangwa pamoja na vijana wengine kujiingiza katika masuala ya uasi kwa hivyo wataweza kuwa moja ya kati ya majeshi ya wanamgambo wa mapinduzi ya serikali,[1] ambao wamedhaminiwa na asasi kivuli inayoongozwa na Jonas Hodges (Jon Voight).[2]

Wakati Jack anafanya kazi za umishonari katika shule ya Okavango huko nchini Sangala, balozi wa Marekani Frank Trammel (Gil Bellows) alimpatia Jack hati ya kuitwa shaurini kuonekana katika Baraza la Seneti la Marekani kuhusiana na mashtaka yake dhidi ya utesaji, lakini alikataa kwenda. Licha ya kusikia kwamba ubalozi utakata msaada wa kifedha unaotelwa kwa ajili ya shule ya Benton iwapo itaendelea kumlinda Jack, akaamua aondoke zake. Muda huohuo, watoto kadhaa waliokuwa wakicheza kabumbu wakavamiwa na jeshi la wa waasi la Juma na kuwateka watoto hao na kuwapa mafunzo ya kijeshi kwa watoto wale. Wakati vijana wawili wamekimbia, askari wale wakafyatua risasi, na kumwua mmoja kati ya wale waliokuwa wakikimbia. Benton akagundua kwamba waasi wanapanga kuishambulia shule yake. Akampigia simu Jack, ambaye aliwaficha watoto chini ya handaki la ndani, na kuua waasi kadhaa kabla ya kukamatwa na kuteswa vibaya-vibaya. Benton akaweza kuwamwacgia cheche wale askari kadhaa waliobakia, na Jack akamuwa kiongozi, Youssou Dubaku (Zolile Nokwe). Kaka'ke, Iké (Hakeem Kae-Kazim) amesikia kifo cha mdogo wake na kupanga njama za kulipiza kisasi, wakati Jack na Benton wanaondoka zao na kuelekea katika ubalozi wa Marekani huko katika mji mkuu kabla helikopta ya mwisho haija ondoka nchini.

Mjini Washington, D.C., Chris Whitley (Kris Lemche) ame-amrishwa na wana-njama waliowezesha jeshi la wanamgambo la Juma kufuta taarifa ambazo zitawatia hatiani. Badala yake, akampigia simu raifiki yake Roger Taylor (Eric Lively), mtoto wa Rais Mchaguliwa Allison Taylor (Cherry Jones), kwa ajili ya msaada. Baada ya Roger kusikia njama za kisiasa, Whitley akarudia zake nyumbani ili azitume zile faili, amezuiliwa na watu wa Hodges pekee, ambaye amezichukua taarifa zile, na kumwua Whitley na kuzika mwili wake na zege.

Jack, Benton na vijana wakamwagiwa cheche na helkopta ya Iké. Wakati wanatorokea misituni, Benton amekanya mabomu ya ardhini. Kwa muda mchache uliobakia ili lilipuke, Benton akamwarakisha Jack aondoke, hivyo anaweza kukawiza wakati. Wakati kazungukwa na Iké na watu zake, Benton ametoa mguu wake na kufyatua bomu lile, na kumwua yeye mwenyewe na waasi, lakini Iké alipona. Jack na watoto waliendelea kuelekea mji mkuu, ambapo Jack aliweza kushinda shambulio jingine la waasi. Getini mwa ubalozi, Trammel amekataa kuingia kwa watoto na kumtishia Jack kwamba atatoa siri zake iwapo hato-salimu amri - kwa usalama wa watoto. Kwa kutotaka, Jack kakubali, kuutoa sadaka uhuru wake. Wakati Taylor anasherekea Urais, Jack na watoto wakaokolewa, na kuacha ghasia nyuma huko Sangala.

Washiriki

[hariri | hariri chanzo]
  1. Eric Goldman (3 Oktoba 2008). "IGN: 24: Redemption Preview". IGN. Iliwekwa mnamo 12 Oktoba 2008.
  2. "24: Redemption". Jon Cassar (director); Howard Gordon (writer). 24 (Fox Broadcasting Company). 23 Novemba 2008.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
24