Nenda kwa yaliyomo

Ziwa Poyang

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ziwa Poyang
Eneo la maji km2 3,210
Kina cha chini m 8-25
Mito inayoingia Mto Gan
Mito inayotoka Mto Gan
Kimo cha uso wa maji
juu ya UB
m 16.5

Ziwa Poyang ndilo ziwa kubwa zaidi la maji safi nchini China. Linapatikana katika Jimbo la Jiangxi. Ziwa hilo linapokea maji yake hasa kutoka mto Gan, pamoja na mito ya Xin na Xiu. Gan inatoka tena ziwani na kupeleka maji yake kwenda mto Yangtze.

Kiasi cha maji kwenye ziwa hilo hubadilikabadilika kufuatana na majira na hivyo ukubwa wake huchezacheza. Kwa sasa ukubwa wa kawaida ni mnamo km2 3210 lakini mwaka 2016 lilipungua hadi kuwa na km2 200 pekee. Lilipungua tangu kuundwa kwa Lambo la Magenge Matatu kwenye mto Yangtse.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ziwa Poyang kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.