Zinduo

Zinduo ya tarakilishi kwenye Linux.
Katika utarakilishi, zinduo (kwa Kiingereza: booting au boot) ni mchakato wa kuzindua tarakilishi.
Kuna aina mbili za zinduo:
- Zinduo baridi ni mchakato wa kuzindua tarakilishi iliyozimwa.
- Zinduo moto ni mchakato wa kuzindua tarakilishi ambayo imewashwa tayari. Zinduo moto inazindua tarakilishi bila kuizima.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- Kiputiputi, O. (2011). Kamusi sanifu ya kompyuta. Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, K.602.