Zakia Mrisho Mohamed

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Zakia Mrisho Mohamed
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwanariadha
Uzito kg 50
Urefu m 1.6

Zakia Mrisho Mohamed (alizaliwa 19 Februari 1984) ni mwanariadha wa mbio za masafa marefu.

Alizaliwa mkoani Singida nchini Tanzania.[1]. Amefanikiwa kushiriki katika mashindano mbalimbali ya riadha ambapo mwaka 2008 na 2012 aliweza kuiwakilisha nchi yake katika mashindano ya Olimpiki kwa kukimbia mbio za mita 5000.

Zakia aliweza kushiriki mashindano ya kimataifa ya riadha kwa mara ya kwanza mwaka 2003,ambapo alikimbia urefu wa mita 3000 na kufanikiwa kuwa nafasi ya sita. Pia mwaka 2004 katika mashindano yaliyojulikana kama "Cinque Mulini", aliweza kuibuka mshindi wa kwanza na kuwa mwanamke Mtanzania wa kwanza kuwahi kutwaa taji hilo.

Alichaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya 2005 IAAF World Cross Country Championships na kushika nafasi ya 20 katika mbio ndefu. Lakini alifanikiwa kuwa nafasi ya sita mbio za mita 5000  kwenye 2005 World Championships in Athletics na mwezi mmoja badae akawa wa tatu katika mashindano ya mbio ya "3rd IAAF World Athletics Final|World Athletics Final" (mita 3000).

Mrisho aliteuliwa kama mmoja wa wakilishi kutoka Afrika kushiriki mashindano ya urefu wa m 5000, kwenye mashindano ya 2010 IAAF Continental Cup akafanikiwa kushika nafasi ya tano.[2]

Mafanikio binafsi[hariri | hariri chanzo]

  • mita 1500 - 4:10.47 (2005)
  • mita 3000 - 8:39.91 (2005)
  • mita 5000 - 14:43.87 (2005)
  • mita 10,000 - 32:20.47 (2010)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Athlete Profile. Demadonna. Retrieved on 2010-09-12.
  2. Marofit take Prague 10Km. IAAF (2010-09-12). Retrieved on 2010-09-12.