Nenda kwa yaliyomo

Zakaria Madole

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Zakaria madole
Amezaliwa 26 julai 1984
Mahoma makulu
Nchi Tanzania
Kazi yake wanamuziki


Zakaria Madole (Dj Mchomo; alizaliwa Mahoma Makulu, Wilaya ya Dodoma Mjini, Mkoa wa Dodoma, Tanzania, 26 Julai 1984) ni mwanamuziki wa Tanzania.

Alisoma shule ya msingi na kumaliza mwaka 1999 katika Kijiji cha Mahoma Makulu na baada ya kumaliza masomo yake ya msingi alijiunga na Sekondari ya D.C.T (Dieces of Central Tanganyika) iliyoko Mvumi katika Wilaya ya Chamwino zamani ikiwa katika Wilaya ya Dodoma Vijijini, pia baada ya hapo alijiunga na Sekondari ya City High School iliyoko mjini Dodoma kwa masomo ya kidato cha Sita.

Baada ya kumaliza masomo yake ya kidato cha sita mwanzoni mwa mwaka 2008 alianza harakati za kutafuta maisha katika mji wa Dodoma na kufanikiwa kukutana na watu mbali mbali ambapo alijikuta akianza kufanya kazi zinazohusika sana na kompyuta kutokana na kwamba mapenzi yake yalikuwepo sana katika utumiaji wa kompyuta na alipenda hata siku moja naye aweze kufanya shughuli zake nyingi kwa kutumia kompyuta.

Hilo alifanikiwa kutokana na kwamba alijikuta akiendesha maisha yake mjini kwa kazi mbali mbali zilizohusu kompyuta basi aliweza kuzifanya pasipo kupitia hata katika chuo kimojawapo kinachofundisha mambo hayo.

Zakaria au Mchomo kama wengi walivopenda kumwita vile vile alikuwa na ndoto nyingi sana za kuja siku moja aweze kuwa mtayarishaji wa muziki au muandaaji wa vitabu mbali mbali vya hadithi ambavyo ni kipaji chake mojawapo cha utungaji wa hadithi na kupiga muziki au kuandaa kama producer.

Baada ya kuona vyote hivo vinahitaji mtaji ama maandalizi makubwa aliamua vile vile kujaribu upande mwingine kwa kutaka kujua zaidi upigaji wa muziki hasa katika kumbi za starehe kama DJ, ndoto yake hiyo ilionesha kutimia baada ya siku moja kukutana na DJ maarufu kipindi hicho mkoani Dodoma aliyekuwa katika ukumbi wa NK au NK CLUB Dj Hans G au GOBOS kama wengi walivopenda kumuita.

Dj Hans G alimkubalia kujifunza muziki katika klabu ile lakini kutokana na kila mtu kubanwa na mambo mengi kwa kipindi kile ikawa imeshindikana kabisa kupatikana muda mzuri wa kufundisha japo maelekezo madogo yalishatolea kuhusiana na matumizi ya kiujumla ya mashine za kupigia muziki.

Safari yake ya U-Dj

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya hapo siku moja Mchomo alikutaka na Meneja wa Club La Aziz na kumwambia lengo lake la kuwa mpigaji wa muziki.. basi meneja yule nae alimpokea vizuri na tokea hapo akakubaliwa kujifunza pale Club La Aziz japo alionesha uwezo mkubwa sana katika upigaji wa muziki kiasi kwamba walio wengi walikuwa wakikataa alipowaambia hajawahi kupiga sehemu nyingine yoyote wala hajawahi kutumia mashine za kupiga muziki popote pale bali ni uwezo binafsi na juhudi zake za kuwa na nia ya kujifunza zaidi.

Kutokana na mambo kuingiliana hakukaa sana club pale na ndipo alipokutana na watu wa Radio moja iliyoitwa Impact Fm ambayo ilikuwa ndo kwanza inafunguliwa katika Mji wa Dodoma hivo pia aliweza kukutana na wahusika na kuwaeleza nia yake kwamba ni Dj mzuri ambaye vile vile ana maktaba ya kujitosheleza katika upande wa nyimbo na ndipo Impact Fm walipomkubalia kwa majaribio madogo na walipouona uwezo wake basi wakawa wamemchukua kuanzia hapo mwanzoni mwa mwaka 2012.

Mnammo mwaka 2014 mwanzoni aliachana na watu wa Radio na kuanza kazi zake binafsi ambapo alikuwa akihusika sana pia na ubunifu wa kutumia kompyuta (Graphics Designer). Kazi hii alikuwa akiifanya toka muda mrefu mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya kidato cha sita. wakati anaendelea na kazi hii alikuwa hana ofisi maalumu kitu ambacho kilimpelekea kutafuta ni namna gani ya kupata ofisi yake ambayo kwa sasa inaendelea na lengo lake kubwa likiwa ni kuwawezesha wakazi wa eneo ama mkoa aliopo hawapati shida tena kwa kutegemea kazi za kutoka Dar es Salaam ambapo ndio mji mkubwa wenye kujitosheleza kwa kila kitu.

Mawazo yake hayo yalianza taratibu huku akiendelea kusimamia na kuiendesha blog yake (http://djmchomo.blogspot.com/)aliyoinzisha makusudi kabisa kwa kuwasaidia wasanii nchini Tanzania ambao walikuwa wakipata shida sana kuzifikisha kazi zao maeneo mbalimbali, aliwapa msaada wa kuwapelekea nyimbo zao maeneo mbalimbali kwa njia ya mtandao ikiwemo radio na watu wedngine vilevile wakiwemo wenye mitandao kwa kuzisambaza pia katika social media.

Mwaka 2015 ni mwaka ambao aliuanza kwa mategemeo makubwa kutimiza malengo yake na ndoto kubwa ikiwa ni kujikamilishia malengo ya kumiliki mitambo itakayomuuwezesha kuzifanya shughuli zake kiurahisi zaidi.

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zakaria Madole kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.