Milima ya Zagros
Mandhari
(Elekezwa kutoka Zagros Mountains)
Milima ya Zagros (kwa Kifarsi: کوههای زاگرس kuh-haye zagros) ni safu ya milima katika magharibi na kusini-magharibi nchini Iran ikienea pia katika Iraki na Uturuki.
Urefu wake ni mnamo kilomita 1,500. Safu inaanza kaskazini-magharibi mwa Iran, ikifuata mpaka wa magharibi wa nchi hiyo halafu pwani ya Ghuba ya Uajemi upande wa kusini, ikiishia kwenye mlangobahari wa Hormuz.
Miinuko ya juu zaidi katika Milima ya Zagros ni Zard Kuh (mita 4,548) na mlima Dena (m 4,359).
Eneo la Zagros ni sehemu muhimu ya uzalishaji wa mafuta ya petroli.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Tovuti za Nje
[hariri | hariri chanzo]- Zagros, Picha kutoka Iran, Livius Archived 21 Novemba 2007 at the Wayback Machine. .
- Major Peaks of the Zagros Mountains
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Milima ya Zagros kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |