Zaghouan
Mandhari
Zaghwan (au Zaghouan; kwa Kiarabu زغوان Zaġwān ?) ni mji kaskazini mwa Tunisia uliopo takriban kilomita 100 upande wa mji mkuu Tunis na km 50 kutoka mwambao wa Bahari ya Mediteranea. Ni makao makuu ya Wilaya ya Zaghouan.
Iko juu ya milima midogo ya Dorsale; kutokana na kimo chake hakina joto kali na hali ya maji ni nzuri. Zamani kulikuwa na mifereji ya juu iliyopeleka maji hadi Karthago.
Mji ni maarufu kwa mashada yake ya maua ya waridi; kilimo hicho kilianzishwa na wakimbizi Waislamu kutoka Hispania katika karne ya 17.
Upande wa kusini mwa mji kuna magofu ya hekalu ya maji ya enzi za Kiroma iliyokuwa mwanzo wa mfereji wa juu wa maji kwenda Karthago.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Postikadi ya Zaghouan mnamo 1900
-
Zaghouan nchini Tunisia
-
Bustani ya Tunisia kwenye mlima Djebel Zaghouan
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Zaghouan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |