Postikadi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Postikadi yenye picha ya meli
Upande wa kinyume mwenye anwandi, stempu ma ujumbe mfupi

Postikadi (ing. post card) ni aina ya barua isiyo na bahasha. Kwa kawaida ni kipande cha kistatili cha karatasi chenye ujumbe mfupi unaotumwa kwa posta.

Mara nyingi postikadi huwa na picha upande mmoja halafu anwani, stempu na ujumbe mfupi upande wa kinyume. Gharama ya postikadi ni kidogo chini ya gharama ya barua katika bahasha.

Ilhali postikadi haina bahasha ujumbe wake unaweza kusomwa na kila mtu anayeishiska. Kadi hizi zilianza kutumiwa kuanzia miaka ya 1860. Tangu kuwa na bei ndogo kuliko barua idadi ya postikadi kati ya barua iliongezeka. Baada ya kupatikana kwa simu za mkononi, sms na barua pepe postikadi zimepungua sana. Bado zinatumiwa hasa na watu waliosafiri wakitaka kutuma picha ya mahali walipofika.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]