Nenda kwa yaliyomo

Mstatili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kistatili)
Mstatili na ulalo zake (nyekundu)

Mstatili ni umbo la pembenne na kila pembe ina 90° yaani ni pembemraba. Pande mbili zinazotazamana ni sambamba pia zina urefu sawa.

Lalo zinalingana na hujigawa sawa pale zinapokutana.

Mraba ni hali ya pekee ya mstatili ambako kila upande ni sawa.

Vitabu, meza, madaftari na karatasi za kuandika kwa kawaida ni umbo la mstatili.


Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mstatili kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.