Nenda kwa yaliyomo

Zachary Levi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Zachary Levi

Zachary Levi, Julai 2014.
Amezaliwa Zachary Levi Pugh
29 Septemba 1980 (1980-09-29) (umri 43)
Lake Charles, Louisiana, Marekani
Kazi yake Mwigizaji, mwimbaji, mwongozaji
Miaka ya kazi 2002–hadi sasa
Tovuti rasmi

Zachary Levi Pugh (amezaliwa tar. 29 Septemba 1980), anafahamika kwa jina lake maarufu kama Zachary Levi, ni mwigizaji wa vipindi vya televisheni, mwongozaji, na mwimbaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa nyusika zake za Kipp Steadman kwenye Less than Perfect, Chuck Bartowski kwenye Chuck, na Flynn Rider kwenye Tangled.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Levi, mtoto wa kati baina ya dada zake wawili waliomtangulia kuzaliwa, alizaliwa mjini Lake Charles, Louisiana, na Bi. Susy na Darrell Pugh.[1] Levi ana asili ya Kiwelisi-Kimarekani.[2]Akiwa mtoto, famili yake imehama mahali chungumzima nchini humo kabla ya kufanya makazi yao ya mwisho huko mjini Ventura, California, ambapo Levi alijiunga katika shule ya Buena High School kwa muda wa miaka minne.[3] Ameanza kuigiza katika tamthilia akiwa na umri wa miaka 6, akicheza nyusika kuu katika matayarisho ya kikanda kama vile Grease, The Outsiders, Oliver, The Wizard of Oz na Big River katika Simi Valley Cultural Arts Center.

Levi anaipigia debe kipindi cha televisheni cha Chuck kwenye San Diego Comic-Con mnamo mwezi wa Julai 2009

Kwa mara ya kwanza alionekana kwenye filamu ya televisheni ya FX, Big Shot: Confessions of a Campus Bookie. Amecheza kama Kipp Steadman kwenye ucheshi wa ABC Less Than Perfect. Pia amecheza uhusika kama kipenzi cha Jane kwenye filamu ya TV ya Charisma Carpenter, See Jane Date. Ambayo inasambazwa na ABC. Levi alichaguliwa kuwa kiongozi kwenye kipengele cha kwanza cha cha ABC kilichoitwa Three kwa ajili ya msimu wa 2004/2005 wa televisheni. Ilitungwa na Andrew Reich akiwa na Ted Cohen, na ilibidi alishiriane na James Van Der Beek, Jama Williamson, na Jacob Pitts, lakini kwa bahati mbaya kipindi hicho hakikuchaguliwa.[4] Levi alisaidia msaada wa kifedha katika albamu ya Kendall Payne ya Grown baada ya kubwagwa na studio yake aliokuwa akifanya nayo kazi, Capitol Records.[5]

Ametua akiwa muhusika mkuu kwenye mfululizo wa TV wa Chuck, mfululizo ambao kwa sasa upo katika msimu wa nne. Levi na mwigizaji mwenzake katika Chuck, Yvonne Strahovski, walibahatika kuchaguliwa katika kategoria ya Best Action Actor na Actress Choice TV Series kwa Teen Choice Awards 2010 ambapo wote walishinda na kuzawadiwa.[6] Katika majira ya joto ya mwaka wa 2008, Levi alitajwa katika orodha ya jarida la Entertainment Weekly ya Top Thirty People Under Thirty.[7] Baadaye akaja kuonekana katika filamu ya Alvin and the Chipmunks: The Squeakquel katika uhusika mkuu akiwa kama binamu wa kina Chipmunks Toby Seville.[8] Pia amecheza na Mandy Moore kwenye filamu ya katuni ya Disney-2010 Tangled, ambayo inatokana na ngano mashuhuri ya Rapunzel. Amecheza sauti ya Flynn Rider, jambazi aliyekuta mkimbizi katika mnara wa Rapunzel. Levi ametia maelezo katika filamu ya mwaka wa 2011 Under the Boardwalk: The Monopoly Story, makala ya tv inayohusu mchezo wa Monopoly.[9]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Filmografia

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Filamu/Vipindi vya Televisheni Nyusika Maelezo
2002 Big Shot: Confessions of a Campus Bookie Adam
2002–06 Less Than Perfect Kipp Steadman (TV series)
2003 See Jane Date Grant Asher (TV Movie)
The Division Todd in "The Box" (sehemu #4.16) na "Hail, Hail, the Gang's All Here" (sehemu #4.19) (TV Series)
2004 Curb Your Enthusiasm Bellman in "Opening Night" (sehemu #4.10)
2005 Reel Guerrillas Evon Schwarz
2006 Big Momma's House 2 Kevin
2007 Spiral Berkeley
Ctrl Z Ben Pillar
2007–present Chuck Chuck Bartowski (TV series)
2008 Wieners Ben
The Tiffany Problem Zac
An American Carol Lab Tech #1
Shades of Ray Ray Rehman
2009 Stuntmen Troy Ratowski
Alvin and the Chipmunks: The Squeakquel Toby Seville
2010 Byron Phillips: Found Byron Phillips
Tangled Eugene Fitzherbert (Flynn Rider) (Voice)
Under the Boardwalk: The MONOPOLY Story Mwadithiaji (Sauti)
2011 Tower Heist Robin "Clyde" Hopkins Filming
Alvin and the Chipmunks: Chip-Wrecked Toby Seville
  1. http://www.tvguide.com/celebrities/zachary-levi/bio/191119
  2. Wyatt, Edward. "Super Nerd Is Out to Save the World", The New York Times, 30 Septemba 2007. Retrieved on 21 Agosti 2010. 
  3. "Anytime with Bob Kushell feat. Zach Levi". Anytime with Bob Kushell. 5 Februari 2009. No. 8, season 1.
  4. Lisotta, Christopher. "SPECIAL REPORT: Upfront Navigator", Television Week, 16 Mei 2005, pp. 32–37. 
  5. Carlozo, Louis R.. "Grown", Christian Century, 4 Aprili 2006, p. 55. 
  6. Stransky, Tanner. "2010 Teen Choice Awards winners announced", 9 Agosti 2010. Retrieved on 8 Machi 2011. 
  7. Markovitz, Adam; Tanner Stransky. "30 Under 30: The Actors", Entertainment Weekly, 3 Machi 2008. Retrieved on 10 Machi 2009. Archived from the original on 2014-04-19. 
  8. Corliss, Richard (11 Januari 2010), "ALVIN AND THE CHIPMUNKS: THE SQUEAKQUEL".Time. 175 (1):51
  9. Wright, Anders. "Rolling the dice", 2 Machi 2011. Retrieved on 25 Machi 2011. Archived from the original on 2012-03-13. 

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zachary Levi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.