Yvonne Nelson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yvonne Nelson

Amezaliwa Yvonne Nelson
Novemba 12, 1985
alizaliwa Accra Ghana,
Nchi Accra Ghana
Kazi yake i mwigizaji, mwanamitindo, mtayarishaji wa filamu na mjasiriamali wa Ghana

Yvonne Nelson (alizaliwa Accra Ghana, Novemba 12, 1985)[1] ni mwigizaji, mwanamitindo, mtayarishaji wa filamu na mjasiriamali wa Ghana.[2]

Amecheza katika sinema kadhaa, pamoja na House of Gold (film) (2013), Any Other Monday, "Mnamo Aprili", na "Swings".[3][4][5]

Maisha ya mapema[hariri | hariri chanzo]

Yvonne Nelson ana asili ya watu wa Fante na watu wa Ga. Alianza masomo yake Shule ya St. Martin De Porres Accra [6] na baadaye akaenda Aggrey Memorial A.M.E. Shule ya Upili ya Sayansi | Aggrey Memorial Senior High School. Alikuwa na elimu ya juu kutoka Chuo Kikuu cha Zenith na [[Chuo Kikuu cha Kati (Ghana) | Chuo , ambapo alifanya kozi ya udhamili ya ( usimamizi wa rasilimali watu).[7][8] Alihitimu kwenye (Taasisi ya Usimamizi na Utawala wa Umma ya Ghana (GIMPA)) na kupata Shahada ya Uzamili katika Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia mnamo 2020.[9]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Nelson, mshiriki wa zamani wa Miss Ghana, alishiriki kwenye maonyesho makubwa.alijulikana kwa uhusika kama Princess Tyra na Playboy. Alitengeneza sinema itwayo The Price, mwaka 2011 . Alizalisha pia Single and Married mnamo 2012 na House of Gold mnamo 2013.[10] Badae alishinda Picha Bora katika Tuzo za Sinema za Ghana na Sinema Bora ya Ghana ya mwaka 2013 City People Entertainment Awards.[11]

Maisha ya binafsi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Oktoba 29, 2017, Nelson alimzaa binti yake Ryn Roberts na mpenzi wake wa zamani, Jamie Roberts.[12] Mwigizaji huyo alikaa kimya juu ya uvumi juu ya ujauzito wake hadi alipotangaza kuzaliwa kwa binti yake kupitia Jalada la Jarida la WOW [13].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yvonne Nelson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.