Nenda kwa yaliyomo

Yemi Osinbajo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yemi Osinbajo


Makamu wa Rais wa Nigeria
Aliingia ofisini 
29 Mei 2015
Rais Muhammadu Buhari
mtangulizi Namadi Sambo

Mwanasheria Mkuu katika Jimbo la Lagos na Kamishna wa Sheria
Muda wa Utawala
1999 – 2007

tarehe ya kuzaliwa 8 Machi 1957 (1957-03-08) (umri 67)
Lagos, Lagos State, Nigeria
utaifa Nigeria
chama All Progressives Congress
ndoa Oludolapo Osinbajo
watoto 3
mhitimu wa
Fani yake Mwanasheria, wakili, mchungaji wa kanisa
dini Ukristo[1]
tovuti profyemiosinbajo.com

Oluyemi Oluleke Osinbajo (* 8 Machi 1957) ni wakili na mwanasiasa nchini Nigeria. Tangu 29 Mei 2015 alikuwa makamu wa rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. Yeye ni pia wakili, mwanasheria aliyefundisha kwenye chuo kikuu alishika vyeo mbalimbali katika idara ya sheria ya Jimbo la Lagos anakotoka. [2] [3]

Maisha ya binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Yemi Osinbajo alizaliwa mwaka 1957 mjini Lagos. Alimwoa Dolapo Soyode Osinbajo aliye mjukuu wa Obafemi Awolowo.[4] Wana watoto watatu.

Yemi Osinbajo alisoma ngazi ya msingi kwake Lagos na 1969–1975 alikuwa kwenye shule ya sekondari ya Igbobi College Yaba, Lagos, Nigeria.[5] 1975–1978 alianza masomo ya sheria kwenye Chuo Kikuu cha Lagos hadi kufikia digrii ya kwanza. Halafu akashiriki katika utumishi wa vijana kwa umma (kama JKT ya Tanzania) kulingana na sheria ya Nigeria alipokuwa mshauri wa kisheria katika mkoa wa Bondel. Kutoka hapo aliendelea kusoma Uingereza kwenye London School of Economics alipopata digrii ya pili ya sheria mwaka 1981.

Mwanasheria

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kurudi aliajiriwa mwaka 1981 kuwa mwalimu wa sheria kwenye Chuo kikuu cha Lagos akaendelea hadi 1986. 1988 - 1992 alikuwa mshauri wa mwanasheria mkuu wa Nigeria.

1997 hadi 1999 alikuwa profesa wa shria na mkuu wa idara ya sheria Lagos. Kutoka hapa aliitwa kuhudumia kama mwanashaeria mkuu mwenye cheo cha waziri katika serikali ya Jimbo la Lagos.

2007 - 2013 alirudi Chuo Kikuu cha Lagos kama profesa. Tangu 2007 aliingia katika kampuni ya mawakili Simmons Cooper Partners (Barristers and Solicitors), Nigeria.[6]

Uchungaji

[hariri | hariri chanzo]

Pamoja na shughuli zake za kisheria Yemi Osinbajo alibarikiwa pia kuwa mchungaji katika Redeemed Christian Church of God, moja kati ya makanisa makubwa ya kipentekoste nchini Nigeria. Amekuwa mchungaji kiongozi wa ushirika wa "Lagos Province 48" inayoitwa pia Olive Tree provincial headquarter parish. Alitangaza ya kwamba aaendelea kushika cheo hiki hata baada ya kuwa makamu wa rais. [6]

Wakati wa kuundwa kwa chama kipya cha All Progressives Congress (APC) mnamo 2013 Yemi aliombwa kutunga ilani ya uchaguzi ya chama na pamoja na wengine alitoa manifesto iliyoitwa "Roadmap to a New Nigeria". Ahadi muhimu zilikuwa milo ya bure kwa wanafunzi shuleni, malipo ya serikali kwa wazazi maskini wakipeleka watoto wao shule na kuwapatia chanjo. Kulikuwa pia na mipango ya kuunda nafasi za kazi kwa vijana.[7]

Mwaka 2014 mgombea wa urais wa All Progressives Congress jenerali mstaafu Muhammadu Buhari alimtangaza Osinbajo kama makamu wake kwa uchaguzi wa 2015. [8][9][10][11]

Baada ya ushindi wa Buhari aliapishwa pamoja na makamu wake tarehe 29 Mei 2015.


  1. "Meet Buhari's running mate, Prof Yemi Osinbajo". Vanguard (Nigeria). 17 Desemba 2014. Iliwekwa mnamo 29 Januari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Democracy Day: Kudos, knocks for Nigeria's judiciary – DailyPost Nigeria". DailyPost.ng. Iliwekwa mnamo 1 Aprili 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Biography". profyemiosinbajo.com. 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-02-05. Iliwekwa mnamo 29 Januari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Ameh Comrade Godwin. "Osinbajo vows never to steal public funds if elected", Daily Post, February 3, 2015. 
  5. "Professor Yemi Osinbajo's Profile", Vanguardngr.com. Retrieved on 4 February 2015. 
  6. 6.0 6.1 "I’m Still a RCCG Pastor, Says Vice President Yemi Osinbajo", connectnigeria. Retrieved on 2017-02-06. Archived from the original on 2015-07-11. "Just like Pastor Ibitayo has said we are on loan. I am still the pastor-in-charge of Province 48 in Lagos and my wife remains wife of the pastor-in-charge."
  7. "APC unveils Manifesto, Code of Ethics – Premium Times Nigeria". Premiumtimesng.com. 6 Machi 2014. Iliwekwa mnamo 1 Aprili 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "Meet Buhari's running mate, Prof Yemi Osinbajo". Vanguardngr.com. 17 Desemba 2014. Iliwekwa mnamo 1 Aprili 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Meet Buhari's Running mate, Prof Yemi Osinbajo". All Progressive Congress. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-28. Iliwekwa mnamo 2017-02-06.
  10. "APC is govt in waiting – Tinubu". The Punch – Nigeria's Most Widely Read Newspaper. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-01-22. Iliwekwa mnamo 1 Aprili 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. NewsPunch. "APC VP Ticket: Tinubu shuns Fashola, Amaechi, others; favours Osinbajo". Newspunch.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-21. Iliwekwa mnamo 1 Aprili 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]