Yael Abecassis

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Yael Abecassis
Yael Abecassis.jpg
Alizaliwa 19 Julai 1967 (1967-07-19) (umri 55)
Ashkelon, Israel
Kazi yake Mwigizaji
Mwanamitindo
Ndoa Lior Miller (1996–2003)
Roni Duek (2005–)

Yael Abecassis (Hebrew: יעל אבקסיס‎ ‎; amezaliwa tar. 19 Julai 1967, Ashkelon, Israel) ni mwigizaji filamu na mwanamitindo kutoka nchini Israel.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Yael Abecassis alizaliwa huko Ashkelon, Israel, kwa wazazi wa kiyahudi wa Moroccan. Abecassis alioana na mwigizaji wa Israel Lior Miller mwaka 1996 na kujaliwa mtoto mmoja. Walitalakiana mwaka 2003. Kwa sasa ameolewa na mjasiriamali Ronny Douek. Abecassis ni binti wa Raymonde Abecassis mwigizaji na mwimbaji wa Israel.[1]

Kazi ya uigizaji na mitindo[hariri | hariri chanzo]

Yael Abecassis alianza uanamitindo akiwa na umri wa miaka 14. Baadae alijikita katika runinga na filamu, akionekana katika matangazo na kuwa mhusika mkuu aliyetambulika kwa jina la Rivka katika filamu ya Kadosh. Ni filamu ya mwaka 1999 ikiongzwa na Amos Gitai. Katika miaka ya tisini, alikuwa mtayarishaji wa vipindi vya watoto katika runinga ya Israel na kutayarisha video za muziki kwa watoto. Mwishoni mwa miaka ya tisini, aliacha kazi ya runinga na kujihusisha na uigizaji.

Filamu alizoigiza[hariri | hariri chanzo]

 • Hunting Elephants (2013), Dorit
 • Prisoners of War (2010), Talia Klein
 • Shiva (2008), Lili
 • Survivre avec les loups (2007)
 • Sans moi (2007), Marie
 • Papa (2005/II), Léa
 • Va, vis et deviens (2005), Yaël Harrari
 • Until Tomorrow Comes (2004), Daughter
 • Alila (2003), Gabi
 • Ballo a tre passi (2003)
 • Haïm Ze Haïm (2003)
 • Miss Entebbe (2003), Elise
 • Bella ciao (2001), Nella
 • Maria, figlia del suo figlio (2000), Mary of Nazareth
 • Kadosh (1999), Rivka
 • Shabatot VeHagim (1999), Ella
 • Passeur d'enfants (1997), Yael
 • L'enfant de la terre promise (1997), Yael
 • L'enfant d'Israel (1997)
 • Hakita Hameofefet (1995)
 • Ha-Yerusha (1993)
 • Zarim Balayla (1993)
 • Sipurei Tel-Aviv (1992), Sharona
 • Pour Sacha (1991), Judith

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yael Abecassis kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
 1. מי את, ריימונד אל בידאוויה? הסרט של יעל אבקסיס על אמה לא חושף.