Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Ukufunzi (Kutaja vyanzo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Utangulizi   Kuhariri   Kuanzisha Makala   Muundo   Viungo vya Wikipedia   Kutaja vyanzo   Kurasa za majadiliano   Kumbuka   Kujisajili    

Vyanzo vya habari ni mahali tunapopata habari zetu za hakika. Katika wikipedia vyanzo hivi vinatakiwa kuonekana maana habari zisizo na vyanzo kuna uwezekano mkubwa wa kuondolewa.

Katika wikipedia yetu mara nyingi si rahisi kuonyesha vyanzo kwa sababu wachangiaji wengi hawana nafasi ya kutumia maktaba mazuri penye majarida na vitabu vya kitaalamu.

Kwa hiyo tutatumia mara nyingi vyanzo visivyo vya Kiswahili hasa Kiingereza. Ni sawa kunakili orodha ya vyanzo kutoka makala ya en:wikipedia. Kuna pia vyanzo vizuri vinavyopatikana mtandaoni.

Tanbihi chini ya ukurasa

Njia nyepesi kuonyesha chanzo cha habari ni tanbihi chini ya ukurasa. Hapa kuna alama kwenye menyu ya uhariri.

Ukibofya hapa unapata <ref>Insert footnote text here</ref>. Sasa andika chanzo badala ya maneno "Insert footnote text here".

Bado hatua moja: chini ya makala mwishoni kabla ya interwiki andika:

===Marejeo=== <references/>

na vyanzo ulivyotaja kwenye mabano vitaorodheshwa hapo.

Kama chanzo chako ni tovuti fanya hivyo:

  • weka kiungo cha nje kwa kubofya alama ya 4 (inayoonyesha tufe la dunia) kwenye menyu. Inaingiza amri (unaweza kutaipu pia)
[http://www.example.com jina la kiungo]
  • andika anwani ya tovuti kwenye mabano mraba, acha nafasi tupu 1,2 halafu ongeza maneno ya maelezo

Usitaje makala mengine ya wikipedia kama chanzo lakini unaweza kunakili vyanzo kutoka huko KAMA VINAFAA.

Viungo vya Nje

Makala mengi ya wikipedia huwa na sehemu mwishoni inayoitwa "Viungo vya Nje".

Hapa tunaweka viungo vya Nje kwa tovuti zenye maana na kukubalika zinazohusu kichwa na yaliyomo ya makala..

Inatosha kutaipi anwani kamili ya tovuti unayotaka kurejea:

http://www.google.com


Jaribu ulichojifunza katika sanduku la mchanga

Endelea kufunzi na Kurasa za majadiliano