Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Mwongozo (Kutaja vyanzo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Utangulizi   Kuhariri   Kuanzisha Makala   Muundo   Viungo vya Wikipedia   Kutaja vyanzo   Kurasa za majadiliano   Kumbuka   Kujisajili    

Vyanzo vya habari ni mahali tunapopata habari zetu za hakika. Katika Wikipedia vyanzo hivyo vinatakiwa kuonekana maana habari zisizo na vyanzo kuna uwezekano mkubwa wa kuondolewa.

Katika Wikipedia yetu mara nyingi si rahisi kuonyesha vyanzo kwa sababu wachangiaji wengi hawana nafasi ya kutumia maktaba nzuri zenye majarida na vitabu vya kitaalamu.

Kwa hiyo tunatumia mara nyingi vyanzo visivyo vya Kiswahili, na hasa vya Kiingereza. Ni sawa kunakili orodha ya vyanzo kutoka makala ya en:wikipedia. Kuna pia vyanzo vizuri vinavyopatikana mtandaoni.

Kumbuka: makala ya wikipedia si vyanzo vinavyokubalika! Lakini unaweza kutumia vyanzo vinavyotajwa katika makala za enwiki.

Tanbihi chini ya ukurasa

Njia nyepesi ya kuonyesha chanzo cha habari ni tanbihi (footnotes) chini ya ukurasa. Hapa kuna alama kwenye menyu ya kuhariri chanzo.

Ukibofya hapa unafungua dirisha la .
Sasa andika chanzo au maelezo mengine katika nafasi yake chini ya maneno "Maandishi ya marejeo".

Bado hatua moja: chini ya makala mwishoni andika:

===Marejeo===

{{marejo}} AU <references/> AU {{reflist}}

Hapo vyanzo ulivyotaja kwenye mabano au maelezo juu vitaorodheshwa chini ya kichwa hicho.

Kama chanzo chako ni tovuti ya intaneti (nje ya Wikipedia) fanya hivyo:

  • weka kiungo cha nje kwa kuandika mabano mraba [ ] - mara moja tu, si mara mbili jinsi ilivyo kwa viungo vya makala nyingine za Wikipedia! Kati ya mabano hayo uingize anwani ya intaneti au URL (unaweza kutaipu pia), kwa mfano [http://www.example.com] (jina la kiungo)
  • andika anwani ya tovuti kati ya mabano mraba, acha nafasi tupu 1,2 kabla ya mabano ya pili halafu ongeza maneno ya maelezo
[http://www.example.com Maelezo yanayoonekana]

Usitaje makala nyingine ya Wikipedia kama chanzo lakini unaweza kunakili vyanzo kutoka huko KAMA VINAFAA. Kwa mengine ona: Msaada: Marejeo na kutaja vyanzo

Marejeo tata kutoka Wikipedia ya Kiingereza

Mara nyingi tukitafsiri makala ya Kiingereza tunakuta marejeo tata ambayo hayawezi kunakiliwa katika swwiki.

Kwa mfano marejeo yanayoonyesha kitu kama <refname= JINAFULANI> texttext<ref> au {{cite rowlett|mdg}} ambacho hakiwezi kunakiliwa katika Wikipedia yetu.

Fanya hivi: Fungua makala ya swwiki na pia ya enwiki iwe kando yake. Kwenye makala ya enwiki fanya rightclick kwenye sehemu ya buluu ya tanbihi (footnotes/reference), ili upate tab ya tovuti inayorejelewa.

Ukiwa kwenye dirisha la "Hariri chanzo" (source edit), kopi URL (anwani ya intaneti) na kuiweka kati ya mabano makali <ref>[xxxxxx yyyy]</ref>. xxxx ni URL unaokopi, yyyy ni matini ya tanbihi kutoka enwiki. Acha nafasi tupu baina xxx na yyy.

Ukitumia "Chanzo" (visual edit) bofya "Cite" halafu Manual na kuchagua Basic. Pale unaweka URL (xxxx) na baada ya kuacha nafasi, unaingiza matini unayotaka kuonyesha katika tanbihi (yyyy).

Viungo vya nje

Makala nyingi za Wikipedia huwa na sehemu mwishoni inayoitwa "Viungo vya nje".

Hapa tunaweka viungo vya nje kwa tovuti zenye maana na zinazokubalika zinazohusu kichwa na yaliyomo ya makala..

Inatosha kutaipi anwani kamili ya tovuti unayotaka kurejea:

http://www.britannica.com/EBchecked/topic/336408/Leonardo-da-Vinci


Jaribu ulichojifunza katika sanduku la mchanga

Endelea kufunzi na Kurasa za majadiliano

Namna ya kutaja vyanzo

  • Kutaja marejeo katika kitabu: Utataja jina la mwandishi, jina la kitabu, mwaka wa kuchapishwa na mahali pake, kampuni ya kuchapisha, ukurasa au kurasa penye habari unazorejelea
  • Kutaja marejeo katika gazeti au jarida: utataja jina la mwandishi (kama lipo), kichwa cha makala, jina la gazeti/Jarida, tarehe yake
  • Kutaja marejeo kutoka intaneti: utataja jina la mwandishi (kama lipo), kichwa cha makala, jina la tovuti, tarehe yake, unaongeza tarehe ulipoangalia tovuti, URL (=anwani ya intaneti). Huwezi kutumia tovuti yoyote. Facebook, twitter na "social media" kwa jumla si vyanzo vinavyofaa kuunda umaarufu au umuhimu wa habari.