Wikipedia:Makala ya wiki/kontena

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wafanyakazi wanafunga kontena pamoja kwenye meli

Kontena (Kiing. container ) ni sanduku kubwa la metali -hasa feleji_ ambayo vipimo vyake vimesanifishwa kwa matumizi ya kimataifa. Kontena hutumiwa kutunza na kusafirisha bidhaa za kila aina kwa meli, lori au reli. Kontena ndogo husafirishwa pia kwa ndege.

Kontena zimepunguza sana kiwango cha kazi na gharama kinachohitajika kusafisha mizigo.

Kontena ya kimsingi ni kontena ya futi 20. Hii inamaanisha ya kwamba urefu wake ni futi 20 (mita 6.058), upana futi 8 (mita 2.438) na kimo cha futi 8.5 (mita 2.591). Aina hii huitwa TEU (=(Twenty-foot Equivalent Unit) ni kama kipimo cha kutaja kiasi cha mizigo meli inaweza kubeba au kiasi kinachopokelwa katika mabandari ►Soma zaidi