Wikipedia:Makala ya wiki/Kontena

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wafanyakazi wanafunga kontena pamoja kwenye meli

Kontena (Kiing. container ) ni sanduku kubwa la metali -hasa feleji_ ambayo vipimo vyake vimesanifishwa kwa matumizi ya kimataifa. Kontena hutumiwa kutunza na kusafirisha bidhaa za kila aina kwa meli, lori au reli. Kontena ndogo husafirishwa pia kwa ndege.

Kontena zimepunguza sana kiwango cha kazi na gharama kinachohitajika kusafirisha mizigo.

Kontena ya kimsingi ni kontena ya futi 20. Hii inamaanisha ya kwamba urefu wake ni futi 20 (mita 6.058), upana futi 8 (mita 2.438) na kimo cha futi 8.5 (mita 2.591). Aina hii huitwa TEU (= twentyfoot equivalent unit) ni kama kipimo cha kutaja kiasi cha mizigo meli inaweza kubeba au kiasi kinachopokelwa katika mabandari. Kontena inaruhusu kubeba mizigo kutoka mahali hadi mahali kwa kutumia usafiri mbalimbali bila kufungua mzigo tena. Kwa hiyo inawezekana kuchukua mzigo ndani ya kontena kiwandani kwa lori, kuihamisha kwa treni hadi bandarini, kuihamisha kwenye meli na kuisafirisha tena kwa lori na reli kwenye nchi inalyolengwa. ►Soma zaidi