Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Makala ya wiki/Jokate Mwegelo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jokate Mwegelo katika ofisi

Jokate Mwegelo ni mwigizaji wa filamu, mjasiriamali na mwanasiasa kutoka nchini Tanzania. Kwenye mwezi wa Julai 2018 aliteuliwa na rais John Magufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe. Jokate vilevile alikuwa mtangazaji na mwimbaji. Mwaka wa 2011, alishinda tuzo ya Zanzibar International Film Festival akiwa kama mwigizaji bora filamu wa kike. Mwaka wa 2017, Mwegelo aliingizwa katika jarida la Forbes katika Forbes 30 Under 30 kutoka Afrika.

Maisha ya awali na elimu

Mwegelo alizaliwa mnamo tarehe 20 Machi, 1987, huko mjini Washington, D.C, ambapo wakati huo wazazi wake walikuwa wanafanya kazi. Alikulia jijini Dar es Salaam, Tanzania...

Jokate hakujulikana kujishughulisha na siasa hadi mwaka 2017 alipoteuliwa na Umoja wa Vijana wa chama cha CCM (UVCCM) kuongoza Idara ya Uahamasishaji na Chipukizi ya umoja huu akiwa kaimu katibu wa idara hii... ►Soma zaidi