Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Makala ya wiki/FIFA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bendera ya FIFA

Shirikisho la Soka Duniani, kifupi FIFA (far. Fédération Internationale de Football Association) ni shirika linalosimamia mambo ya mpira wa miguu kimataifa. Kisheria ni shirika binafsi lililoandikishwa huko Uswisi. Makao makuu yapo Zurich. Rais ni Joseph Blatter. FIFA inasimamia mashindano ya kimataifa, hasa Kombe la Dunia la FIFA kama mashindano ya pekee kwa wanaume na wanawake. FIFA ilianzishwa mwaka 1904 mjini Paris, Ufaransa na kwa mwaka 2015 ina shirika za kitaifa wanachama 208. Lugha rasmi ni Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani na Kihispania. ►Soma zaidi