Wiski
Wiski (kutoka Kiingereza: whisky au whiskey) ni kinywaji cha alikoholi kilichotengenezwa kutokana na nafaka kikikaa kuiva katika mapipa ya mbao.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Jina la wiski lina asili katika Kikelti cha Ueire; jinsi ilivyokuwa kote Ulaya, ukenekaji wa maji ya matunda na mchanganyiko wa nafaka na maji uliochachuka ulienezwa na wamonaki, mwanzoni kama dawa, baadaye pia kama kinywaji[1]. Wamonaki waliliita tokeo la ukenekaji kwa Kilatini "aqua vitae" yaani "maji ya uhai" , na "whiskey" ni tafsiri tu ya jina hili katika lugha ya Kikelti ya Ueire[2].
Rangi na ukali
[hariri | hariri chanzo]Jinsi ilivyo na vileo vyote vinavyopatikana kwa njia ya ukenekaji, kimiminiko kinachotoka hakina rangi. Wiski inapata rangi yake ya kikahawia kwa kuitunza kwa miaka katika mapipa ya mbao[3].
Wiski hukenekwa kwa usafi wa asilimia 80-94, kutegemeana na sheria za nchi. Baadaye maji yanaongezwa ikiuzwa kwa kawaida ikiwa na kiwango cha alikoholi kisichopungua asilimia 40.
Asili
[hariri | hariri chanzo]Asili ya wiski ni Ueire na Uskoti. Huko inatengenezwa kwa nafaka ya shayiri. Baada ya kuhamia Marekani, watu kutoka nchi hizo walianza kutengeneza kinywaji kwa kutumia nafaka nyingine kama ngano au mahindi.
Wiski nyingi hutengenzwa Uskoti (inapoandikwa whisky)[4] na Ueire (inapoandikwa whiskey) na kuuzwa kote duniani; katika nchi za Ulaya kuna masharti ya kisheria kuhusu kinywaji kinachouzwa kwa jina wiski.
Wiski za Marekani huitwa "bourbon" kutokana na wilaya ya Bourbon katika Jimbo la Kentucky. Lakini siku hizi hutengenezwa katika nchi nyingi, isipokuwa kuna nchi ambako kile kinachouzwa kama "wiski" ni mchanganyiko wa vileo mbalimbali.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ The History of Whisky History Archived 25 Januari 2010 at the Wayback Machine, The Whisky Guide.
- ↑ New English Dictionary on Historical Principles, entries for "usquebaugh" and "whisky".
- ↑ Stone, Jason (18 Julai 2012). "Whiskey 101". The Whiskey Still Company. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-03-19. Iliwekwa mnamo 14 Julai 2017.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Scotch Whisky Association. "Scotch Whisky Exports Hit Record Level". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Mei 2013. Iliwekwa mnamo 12 Juni 2013.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wiski kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |