Nenda kwa yaliyomo

Seli nyekundu za damu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wekundu wa damu)

Seli nyekundu za damu (pia erithrosaiti , kutoka Kiingereza red blood cells au erythrocyte) ni seli za damu zenye rangi nyekundu.

Kazi yake ni hasa kubeba oksijeni kutoka mapafu kwenda mwilini mwote.[1][2] Seli nyekundu za damu hupokea oksijeni katika mapafu na kuachana nayo wakati zinabanwa katika mishipa ya damu midogo mwilini.

Rangi nyekundu inatokana na protini ya hemoglobini ndani yake.

Damu ya wanawake huwa na seli nyekundu milioni 4.8 kwa mikrolita ya damu. Damu ya wanaume huwa na seli milioni 5.4 kwa ml.[3]

  1. Bradfield, Phil; Potter, Steve (2009). Edexcel IGCSE Biology Student Book. Pearson Education. ISBN 9780435966881.
  2. Liang, Barbara. "General Anatomy & Physiology: Red Blood Cells". Wisc-Online. Iliwekwa mnamo 2011-03-22.
  3. http://www.webmd.com/a-to-z-guides/complete-blood-count-cbc?page=3
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Seli nyekundu za damu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.