Wawakilishi wenye kura
Mandhari
Mwakilishi mwenye kura (elector) ni mtu anayeteuliwa kupiga kura kwa niaba ya wengine. Huchaguliwa katika mfumo wa kisiasa wa nchi mbalimbali kwa uchaguzi usio wa moja kwa moja.
Mifano ni
- wawakilishi wenye kura wanaopiga kura katika baraza maalum (electoral college) inayomchagua raisi wa Marekani. Wanachaguliwa kijimbo na raia wote wenye haki ya kupiga kura. Wanakutana kijimbo kuwapigia kura wagombea wa uraisi; kura zao zinatumwa kwa senati ya Marekani ambako zinajumlishwa na mwenye kura nyingi anatangazwa kuwa rais mpya. Wawakilishi hugombea kwa ajili ya mgombea fulani wa uraisi na kufuatana nasheria za nchi hiyo wanatakiwa kumpa kura yao.
- Wawakilishi wenye kura wanaomchagua raisi wa Ujerumani; hao ni wabunge wote wa bunge la Ujerumani (Bundestag) pamoja na idadi sawa ya wawakilishi wanaoteuliwa na mabunge ya majimbo ya shirikisho wakikutana katika baraza la shirikisho (federal convention, Bundesversammlung)[1]
- Nchini Ufaransa ndio wawakilishi wa mabunge ya wilaya (département), mabunge ya mikoa (région) na mabunge ya miji na tarafa za Ufaransa, kwa jumla takriban wawakilishi 15,000, wanaokutana kiwilaya na kupigia kura wabunge wa senati ya Ufaransa ambayo ni "chumba cha juu" cha bunge la nchi hiyo.
- Nchini Italia wabunge wa vitengo vyote viwili vya bunge, pamoja na idadi ya wawakilishi wa mikoa ya nchi humpigia kura rais wa Italia.
- Pale Burundi[2] na Madagaska[3] wabunge wa senati huchaguliwa na wawakilishi wa mabunge ya tarafa ya nchi
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.bundestag.de/en/parliament/function/federal_convention/federal_convention-201836
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-28. Iliwekwa mnamo 2021-01-21.
- ↑ https://www.business-standard.com/article/pti-stories/madagascar-finally-elects-senate-after-2009-coup-115123000064_1.html
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- "A Handbook of Electoral System Design Archived 24 Desemba 2009 at the Wayback Machine." from International IDEA
- A New Nation Votes: American Election Returns 1787–1825