Wanamazingaombwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wanamazingaombwe ni watu wanaoendesha michezo ya kumfanya mtu aone kitu tofauti na kile kinachofanyika au kwa jina lingine kiinimacho.

Kwa mfano unaweza kuona mwanamazingaombwe anamchunja mtu mbele ya umati wa watu lakini baada ya muda kidogo unamuona mtu yuleyule anatembea akiwa hana hata jeraha.

Hali hii imekuwa ikihusiswha na imani za kishirikina. Hata hivyo, baadhi ya washiriki wa michezo hiyo wamekuwa wakitamba kuwa hawatumii ndumba za aina yoyote ile ila ni ujuzi na kipaji walichonacho.