Vladimir Shubin
Vladimir Gennadievich Shubin (kwa Kirusi Владимир Геннадиевич Шубин; amezaliwa tarehe 9 Julai 1939) ni mwanahistoria wa Urusi anayejishughulisha historia ya Afrika na pia aliyekuwa kiongozi wa tawi mojawapo la Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Umoja wa Kisovyeti[1].
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1962 alihitimu katika Chuo Kikuu cha Moscow cha Mahusiano ya Kimataifa cha Wizara ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Kisovyeti (MGIMO) akapata shahada ya awali ya mahusiano ya kimataifa na baadaye akafanya kazi kwenye Kamati ya Mashirika ya Kimataifa ya Umoja wa Kisovyeti. Miaka 1962-1969 alihudumia Jeshi la Kisovyeti.
Miaka 1969-1979 alikuwa katibu myeka na mkuu wa idara katika Kamati ya Kisovyeti ya Mshikamano wa Nchi za Asia na Afrika. Kuanzia mwaka 1982 hadi mwaka 1991 alikuwa katibu myeka, naibu kiongozi na hatimaye kiongozi wa tawi mojawapo la Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Umoja wa Kisovyeti.
Mwaka 1982 alipata digrii ya uzamivu wa historia baada ya kutetea tasnifu katika Taasisi ya Elimu Utu ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Umoja wa Kisovyeti. Mwaka 1999 akatetea tasnifu kwenye Taasisi ya Nchi za Asia na Afrika na kupata digrii ya udaktari wa historia.
Kuanzia mwaka 2003 yeye ni profesa wa Kitivo cha Historia, Taaluma za Kisiasa na Sheria cha Chuo Kikuu cha Urusi cha Elimu Utu (RSUH). Pamoja na hayo anafanya kazi katika Taasisi ya Afrika ya Chuo cha Sayansi cha Urusi.
Tangu mwaka 2002 yeye ni mshauri wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Baraza la Juu la Bunge la Urusi.
Miaka 1993-2011 alitoa mihadhara katika vyuo vikuu kadhaa vya Afrika, Asia na Ulaya.
Bw. Shubin ni mhariri wa Jarida la Politicon linalochapishwa na Jumuiya ya Taaluma za Kisiasa ya Afrika Kusini (kuanzia mwaka 1998), Jarida la Scientia Militaria (tangu mwaka 2010), Jarida la Asia na Afrika leo mjini Moscow pamoja na Jarida la Globalization Studies huko Volgograd.
Maandishi makuu
[hariri | hariri chanzo]Bw. Shubin aliandika zaidi ya insha 140 za kisayansi ikiwemo ni vitabu 5 vya peke yake.
- «Африканский национальный конгресс в годы подполья и вооруженной борьбы» (М., 1999),
- «Международная социал-демократия и борьба против колониализма и апартеида» (М., 1985),
- «Social Democracy and Southern Africa» (M., 1989),
- «Reflections on Relations between the Soviet Union/Russian Federation and South Africa in 1980s and 1990s» (Bellville, 1994),
- «Flinging the Doors Open: Foreign Policy of the New South Africa» (Bellville, 1995),
- «ANC: a View from Moscow» (Bellville, 1999).
- «Китай и Южная Африка: эволюция взаимоотношений» (М., 1999),
- «Африка: поиск идентичности» (М., 2001.)
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Nishani ya Nyote Nyekundu, Nishani ya Masahaba wa O. R. Tambo (Fedha) na medali 8.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Vladimir Gennadievich Shubin "65468226". viaf.org. Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Wasifu wake katika tovuti ya Taasisi ya Afrika ya Chuo cha Sayansi cha Urusi
- Vladimir Shubin katika tovuti ya Chuo Kikuu cha Urusi cha Elimu Utu (RSUH)