Nenda kwa yaliyomo

Viza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Viza ya Marekani.

Viza (kutoka Kiingereza "visa") ni kibali cha kumruhusu mwenye pasipoti kuingia na kukaa katika nchi geni kwa muda maalum.

Asili ya neno iko katika lugha ya Kilatini ambapo "visum" inamaanisha "imeangaliwa" kwa maana ya kwamba afisa wa serikali ya nchi geni aliona kitambulisho cha mtu na amekubali safari yake. Kiingereza "visa" ni umbo tofauti la Kilatini hiki.

Umbo la viza

[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida viza ni mhuri maalum uliogongwa katika pasipoti. Siku hizi nchi mbalimbali hutumia karatasi za kubandikia katika pasipoti kwa gundi zikilenga kuepukana na mihuri bandia. Nchi chache hutumia viza elektroniki ambako kibali kipo kwenye kompyuta tu, hakionekani tena katika pasipoti.

Viza hutolewa na ubalozi wa nchi kwa kawaida pamoja na malipo ya ada. Inataja aina ya ziara kama ni ya kitalii, ya kibiashara au kwa madhumuni maalum pamoja na muda. Nchi nyingi hutoa vibali kwa miezi mitatu.