Nenda kwa yaliyomo

Kuzingira Yorktown

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Vitu vya Yorktown)

Kuzingira Yorktown (au kuzingirwa kwa Yorktown) kulikuwa tukio la mwisho la Vita vya Uhuru wa Marekani. Mapigano hayo yalianzia tarehe 28 Novemba 1781, na kumalizika tarehe 19 Oktoba 1781[1] yakitoa ushindi kamili kwa nguvu ya washirika Jeshi la Ufaransa na Jeshi la Bara la Amerika. Ushirikiano huo uliongozwa na Jenerali George Washington na Jenerali Rochambeau wa Ufaransa.[2] Wanajeshi wa Marekani na Ufaransa walipigana dhidi ya askari kutoka Uingereza na Ujerumani walioongozwa na Jenerali Charles Cornwallis.[3] Karibu askari elfu thelathini walishiriki. Marekani ilizaliwa kama nchi mpya. Historia ya dunia ilibadilika milele.

Kabla ya kuzingira Yorktown

[hariri | hariri chanzo]

Vita vya Yorktown vilisababishwa kampeni ndefu na mafanikio Marekani katika majimbo ya kusini.[4] Jeshi la Uingereza lilishinda vita hivi kwa miaka sita ya kwanza, lakini kwa sababu wanajeshi wa Uingereza walikuwa wanapigana kupitia Bahari ya Atlantiki hii ilifanya vita hivi kuwa changamoto kwao. Kwa sababu hiyo, Jeshi la Bara la Marekani lilipata ushindi polepole dhidi ya Jeshi la Uingereza. Ushindi huo lilianzia kusini. Kwa sababu ya maendeleo ya Marekani, mfalme wa Ufaransa aliwatuma wanajeshi elfu tano mia tano mwaka wa 1780 kumsaidia Jenerali George Washington.[5] Mfalme wa Ufaransa alitumia nafasi hiyo kuwaumiza adui zake kwa kuwasaidia wanajeshi wa Jeshi la Bara la Marekani. Msaada huo kutoka kwa wanajeshi wa Ufaransa ulisaidia kutega jeshi la Uingereza katikati ya Marekani. Kati ya mwaka 1780 na 1781, jeshi la Ufaransa na Marekani walisukuma jeshi la Uingereza kusini ndani ya jimbo la Virginia.[6] Mashambulizi hayo, pamoja na mafanikio ya Marekani upande wa kusini yaliweka jeshi la Uingereza katika Chesapeake Bay. Pande zote walihitaji ushindi kumaliza vita. Nje ya kijiji cha Yorktown, jeshi la Marekani lilitega jeshi la Uingereza. Kwa usaidizi wa jeshi la wanamaji la Ufaransa wanajeshi wa Marekani waliweza kuwazuia wanajeshi wa Uingereza kupata uimarishaji wa wanajeshi wengine. Jeshi la Uingereza waliangamizwa.

Kuzingira

[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 28 Septemba 1781, jeshi la Marekani na Ufaransa lilizingira jeshi la Uingereza lote kabisa.[7] Jeshi la Marekani na Ufaransa lilikuwa na askari elfu kumi na tisa na jeshi la Uingereza lilikuwa na askari elfu tisa.[8] Jeshi la Uingereza lilichimba mahandaki na kutengeneza ulinzi mwingine. Kwa muda wa wiki mbili, jeshi la Marekani na Ufaransa lilishambulia kwa mabomu mahali pa Uingereza. Mizinga mikubwa na askari wa miguu walitumika tena na tena dhidi ya jeshi la Uingereza. Tarehe 17 Oktoba 1781, Jenerali Cornwallis alituma ofisa nje ya mahali jeshi la Uingereza lilipokuwa na alikubali kusalimu amri bila ya masharti.[9] Kwa siku mbili zijazo, pande zote walikubaliana katika masharti ya kusalimu amri. Tarehe 19 Oktoba, jeshi la Uingereza lilisalimu amri misimamo yao.[10] Kampeni kuu kwenye vita ilikuwa ya ndefu, lakini mwisho wa vita ulikuwa wa haraka.

Baada ya kuzingira

[hariri | hariri chanzo]

Katika mwisho mwa vita, majeruhi walikuwa karibu elfu tisa kwa jeshi la Uingereza na chini ya mia nne kwa jeshi la Marekani na Ufaransa. Baada ya kuangamizwa kwa jenerali mkuu na wanajeshi wengi wa Uingereza serikali ya Uingereza ilianza kuwaondoa wanajeshi wake kutoka bara la Marekani. Wiki tano baadaye habari ilifikia bunge la Uingereza, na hapo waziri mkuu alisema “Mungu wangu, tumekwisha.”[11] Vita hivyo vilisitishwa lakini Mkataba wa Paris haukusainiwa hadi miaka miwili baadaye.

  1. History com Editors. "Battle of Yorktown". HISTORY (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-12-11. {{cite web}}: |author= has generic name (help)
  2. History com Editors. "Battle of Yorktown". HISTORY (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-12-11. {{cite web}}: |author= has generic name (help)
  3. "Yorktown". American Battlefield Trust (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-12-11.
  4. "Siege of Yorktown | Summary, Combatants, Casualties, & Facts | Britannica". www.britannica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-12-11.
  5. Travis Shaw Travis Shaw is a native Maryl, er with a deep love of local history Wanting to share this love with others he received a BA in History from St Mary’s College of Maryl, an MA in Public History from American University His professional career includes nearly two decades of experience in the (2021-01-06). "France in the American Revolution". American Battlefield Trust (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-12-11.{{cite web}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  6. History com Editors. "Battle of Yorktown". HISTORY (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-12-11. {{cite web}}: |author= has generic name (help)
  7. History com Editors. "Battle of Yorktown begins". HISTORY (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-12-11. {{cite web}}: |author= has generic name (help)
  8. "Yorktown". American Battlefield Trust (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-12-11.
  9. "Yorktown". American Battlefield Trust (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-12-11.
  10. "Yorktown". American Battlefield Trust (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-12-11.
  11. "Fix Bayonets: The Revolution's Climactic Assault at Yorktown". American Battlefield Trust (kwa American English). 2018-04-13. Iliwekwa mnamo 2022-12-11.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kuzingira Yorktown kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.