Nenda kwa yaliyomo

Visiwa vya Jumeirah

Majiranukta: 25°03′29″N 55°09′13″E / 25.05800°N 55.15368°E / 25.05800; 55.15368
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
—— Jamii ya United Arab Emirates ——
Visiwa vya Jumeirah

Muono kutoka Angani wa Visiwa vya Jumeirah

Nchi United Arab Emirates
Emirate Dubai
Mji Dubai
Ilopoanzishwa 2004
Takwimu za Jamii
Ukubwa 2.74 km²
Majamii Jirani Emirates Hills, Jumeirah Lake Towers
Stesheni ya Reli ya Dubai Metro       Jumeirah Islands 
Nambari za Uratibu 25°03′29″N 55°09′13″E / 25.05800°N 55.15368°E / 25.05800; 55.15368

Visiwa vya Jumeirah (Kiarabu: |جزر الجميرا )ni makazi ya kifahari mjini Dubai, United Arab Emirates, iliyojengwa na Nakheel moja ya makampuni kubwa zaidi za ujenzi Dubai. Visiwa vya Jumeirah vina visiwa vidogo (viitwavyo nguzo), kila kilicho na manyumba 16 ya kifahari. Visiwa hivi vyote vimejengwa katika ziwa bandia. Ziwa lenyewe ni kubwa hadi muundo huu wote una uwiano wa ardhi kwa maji wa 23:77 [1]


Muundo huu unajumuishwa na visiwa 50 (46 ambavyo ni nguzo za makazi), mkahawa na supamaketi eneo la zoezi, na eneo la burudani. Kila ya nyumba 736 zilizopo ziko na dimbwi la kuogelea na chumba cha mjakazi, na ziko na ujubwa kuanzia futi 5101 hadi 7,200 (670 m2). Mradi ulitimizwa mwisho wa mwaka 2006. Miradi iliyoko karibu ni pamoja na Jumeirah Lake Towers na Palm Jumeirah zote ambazo zinajengwa pia na Nakheel.

  1. [2] ^ Ukweli kuhusu visiwa vya Jumeirah Ilihifadhiwa 29 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.


Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]