Víctor Valdés

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Valdes akiidakia Barcelona mwaka 2001.

Víctor Valdés Arribas (alizaliwa 14 Januari 1982) ni kocha wa mpira wa miguu wa Hispania na mchezaji wa zamani wa Barcelona, yeye alicheza kama golikipa. Kwa sasa yeye ndiye msimamizi wa timu ya FC Barcelona ya 'Juvenil A'.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alitumia muda mwingi wa taaluma yake na Barcelona ya La Liga, na anachukuliwa kuwa mmoja wa magolikipa bora katika historia ya klabu, akiwa ameonekana katika michezo 525 ya klabu na kushinda mataji makubwa 21, ikiwa mataji sita ya La Liga na matatu ya UEFA champions league yaani Mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Kimataifa, Alikuwa sehemu ya kikosi cha Hispania kilichoshinda Kombe la Dunia la 2010 na UEFA Euro 2012, na pia alishiriki kwenye Kombe la Shirikisho la FIFA la 2013, ambapo Hispania ilimaliza katika nafasi ya pili.


Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Víctor Valdés kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.