Uzamivu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Uzamifu)
Jump to navigation Jump to search

Uzamivu (pia PhD ambayo ni kifupi cha Kilatini "Philosophiae Doctor" yaani "Daktari wa falsafa") ni shahada ya juu kabisa katika elimu.

Inatolewa na vyuo vikuu baada ya digrii ya bachelor na shahada ya uzamili.

Kwa kufuata tabia za lugha nyingine, jina daktari hutumiwa pia kama jina la heshima kwa mtu aliyepata shahada ya uzamivu.

Ilikuwa desturi hadi leo kwamba mgombea wa uzamivu anaonyesha uwezo wake kwa kutunga tasnifu ambayo ni kitabu kamili. Siku hizi masharti ya tasnifu zinaweza kutimizwa pia kwa kutunga idadi fulani za makala zinazohitaji kupokewa na majarida ya kitaalamu ambamo zinachunguliwa na wataalamu wengine kabla ya kupokewa na kuchapishwa.

Nuvola apps bookcase.svg Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uzamivu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.