Uwanja wa michezo wa Klabu ya Al Masry

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa michezo wa Klabu ya Al Masry

Uwanja wa michezo wa Klabu ya Al Masry pia unajulikana kama a kwa jina la Port Said Stadium, ni uwanja wa michezo unaotumika kwa matumizi mengi unaopatikana Al Manakh nchini Misri, ulifunguliwa mwaka 1955 na Hussein el-Shafei, waziri wa maswala ya kijamii wa nchi ya Misri kwa niaba ya raisi Gamal Abdel Nasser.

Uwanja wa Klabu ya Al Masry unamilikiwa na Klabu ya michezo ya Al-Masry SC, na una uwezo wa kuingiza idadi ya watu 18,000.Uwanja huo ulisitishwa matumizi yake mnamo tarehe 1 Februari 2012 baada ya matukio ya ghasia katika uwanja huo kufuatia mechi ya Ligi kuu ya mwaka 2011-2012 kati ya timu ya Al Masry na Al Ahly SC ambapo ghasia hiyo ilipelekea vifo vya watu 72 ambao ni mashabiki wa timu ya Al Ahly , na mshabiki mmoja wa timu ya Al Masry pamoja na polisi mmoja.[1] .

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "In pictures: Jubilation in Cairo, riots in Port Said". 26 January 2013. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-02. Iliwekwa mnamo 2021-06-08.  Check date values in: |date= (help)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Klabu ya Al Masry kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.