Uwanja wa michezo wa Casablanca

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa Casablanca

Uwanja wa michezo wa Casablanca ni jina lililopendekezwa na chama cha mpira wa miguu kwa uwanja utakaojengwa huko Casablanca nchini Moroko. Mara baada ya kukamilika mwaka 2025, utatumika zaidi kwa mechi za mpira wa miguu na utatumika kama uwanja wa nyumbani kwa timu ya taifa ya Moroko. Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kubeba idadi ya mashabiki 93,000, na kuufanya kuwa uwanja wa tatu wa mpira wa miguu wa juu zaidi barani Afrika. Ukimalizika, Utachukua nafasi ya Stade Mohamed V.

Muhtasari[hariri | hariri chanzo]

Wazo la awali la uwanja huu lilikuwa la kutayarisha Kombe la Dunia la FIFA la mnamo mwaka 2010, ambapo Moroko walipoteza kwa Afrika Kusini. Hii ilijumuisha viwanja vikuu vitano kote nchini, pamoja na Uwanja wa michezo wa Tanger, Uwanja wa michezo wa Marrakech na vingine viwili katika miji mikubwa ya Agadir na Fes. Ilikuwa moja ya viwanja vyenye kuzabuni Moroko kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la FIFA mnamo mwaka 2026]. Pangechezewa mechi za kuzindua na fainali kama Moroko wangepewa kutayarisha Kombe la Dunia lakini ikashindwa kwa Zabuni ya Umoja ya Kanada, Mexico, na Marekani. Sasa inajipanga kuwania kutayarisha Kombe la dunia la FIFA ya mwaka 2030.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Casablanca kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.