Uwanja wa Buffalo City

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa Buffalo City

Uwanja wa michezo wa mji wa buffalo ambao hujulikana pia Kama BCM Stadium ni uwanja wa michezo unaopatikana katika nchi ya Afrika Kusini, na mara nyingi hutumika kwa ajili ya michezo ya Rugby na hutumika kama uwanja wa nyumbani wa timu ya Border Bulldogs, ukiwa na uwezo wa kuchukua takribani watu 16,000. Kwa mara kadhaa uwanja huu umekuwa ukibadilishwa jina, jina lake la mwanzo ulikuwa ukijulikana kama Border Rugby Union Grounds, Kwa sababu ya ufadhili, uwanja huu ulibadilishwa jina tena na kuitwa ABSA STADIUM .[1][2] Mnamo tarehe 26 Juni 2010,uwanja huu ulitumika kwa ajili ya mechi za majaribio za timu ya taifa ya Italia na Afrika Kusini na iliibuka na ushindi wa magoli 55 kwa 11.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Craven Week in History (25 juni 2010). Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-07-08. Iliwekwa mnamo 2021-06-06.
  2. Absa Stadium. BuffaloCity.gov.za (Oct 13, 2009).
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa Buffalo City kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.