Uvimbe wa aorta ya tumbo
Uvimbe wa aorta ya tumbo | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Upasuaji wa mishipa ya damu |
Dalili | Hakuna maumivu, maumivu ya fumbatio, mgongo, au mguu[1][2] |
Muda wa kawaida wa kuanza kwake | Wanaume wa zaidi ya miaka 50[1] |
Sababu za hatari | Kuvuta sigara, shinikizo la juu la damu, magonjwa mengine ya moyo au mishipa ya damu, historia ya familia, ugonjwa wa Marfan[1][3][4] |
Njia ya kuitambua hali hii | Picha za uchunguzi wa kitabibu kipenyo cha (aorta ya tumbo cha zaidi ya sentimita 3 )[1] |
Kinga | Kuto vuta sigara, kutibu viashiria vya hatari[1] |
Matibabu | Upasuaji (upasuaji wa wazi au matibabu ya uvimbe (aneurismu) kwa njia ya ndani ya mshipa)[1] |
Idadi ya utokeaji wake | ~5% (wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 65)[1] 5M:F[5] |
Vifo | Uvimbe wa aorts wa 167,000 (2017)[6] |
Uvimbe wa aorta ya tumbo (Abdominal aortic aneurysm)[7] ni upanuzi wa kimahali wa aota kwenye eneo la tumbo hivi kwamba kipenyo chake ni kikubwa kuliko sentimita 3 au zaidi ya 50% kubwa kuliko kawaida.[1] Kwa kawaida, hali hii haisababishi dalili, isipokuwa wakati wa kupasuka kwake.[1] Mara kwa mara, maumivu ya tumbo, nyuma, au mguu yanaweza kutokea.[2] Uvimbe (aneurismu) mkubwa wakati mwingine unaweza kuhisiwa kwa kusukuma kwenye tumbo.[2] Kupasuka kunaweza kusababisha maumivu kwenye tumbo au mgongo, shinikizo la chini la damu, au kupoteza fahamu, na mara nyingi kusababisha kifo.[1][8]
Uvimbe wa aorta ya tumbo hutokea kwa kawaida kwa wale walio na umri wa zaidi ya miaka 50, kwa wanaume, na kati ya wale walio na historia ya familia.[1] Sababu za ziada za hatari ni pamoja na uvutaji sigara, shinikizo la damu na magonjwa mengine ya moyo au mishipa ya damu.[3] Hali za kijeni zilizo na hatari iliyoongezeka ni pamoja na ugonjwa wa Marfan na ugonjwa wa Ehlers-Danlos.[4] Uvimbe wa aorta ya tumbo ni aina ya kawaida ya kuvimba kwa aota.[4] Takriban 85% hutokea chini ya figo na hali zinginezo katika eneo la figo au juu yake.[1] Ugonjwa huu wakati mwingine hupatikana wakati wa kuchunguza shida nyinginezo.[5] Nchini Marekani, uchunguzi wa ultrasound ya tumbo unapendekezwa kwa wanaume kati ya umri wa miaka 65 na 75 na wenye historia ya kuvuta sigara.[9] Nchini Uingereza na Uswidi, uchunguzi wa wanaume wote wenye umri wa zaidi ya miaka 65 unapendekezwa.[1][10] Mara baada ya kuvimba huku kupatikana, uchunguzi wa mawimbi ya sauti (ultrasound) zaidi ni kawaida kufanyika mara kwa mara.[2]
Kutovuta sigara ndio njia bora ya kuzuia ugonjwa huo.[1] Njia zingine za kuzuia ni pamoja na kutibu shinikizo la juu la damu, kutibu kolesteroli ya juu ya damu, na kutokuwa na uzito kupita kiasi.[1] Upasuaji kawaida hupendekezwa wakati kipenyo cha uvimbe wa aorta ya tumbo kinakua zaidi ya sentimita 5.5 kwa wanaume na zaidi ya sentimita 5.0 kwa wanawake.[1] Sababu nyingine za kutengeneza ni pamoja na kuwepo kwa dalili na ongezeko la haraka la ukubwa wa mtu, linalofafanuliwa kuwa zaidi ya sentimita moja kwa mwaka.[2] Urekebishaji unaweza kufanywa kwa upasuaji wa wazi au ukarabati wa uvimbe wa mishipani (EVAR).[1] Ikilinganishwa na upasuaji wa wazi, ukarabati wa uvimbe wa mishipani una hatari ndogo ya kifo katika muda mfupi na kukaa kwa muda mfupi hospitalini, lakini huenda lisiwe chaguo bora kila wakati.[1][11][12] Inaonekana hakuna tofauti katika matokeo ya muda mrefu kati ya tiba hizo mbili.[13] Taratibu za kurudiarudia zinahusishwa zaidi na ukarabati wa uvimbe wa mishipani.[14]
Uvimbe wa aorta ya tumbo huathiri 2-8% ya wanaume walio na umri wa zaidi ya miaka 65[1] na unaonekana mara tano zaidi kwa wanaume.[5] Kwa wale walio na uvimbe wa chini ya sentimita 5.5, hatari ya kupasuka katika mwaka ujao ni chini ya 1%.[1] Miongoni mwa wale walio na uvimbe kati ya sentimita 5.5 na 7, hatari ni karibu 10%, wakati kwa wale walio na uvimbe zaidi ya sentimita 7 hatari ni karibia 33%.[1] Vifo vinavyohusiana na kupasuka ni 85% hadi 90%.[1] Katika mwaka wa 2017, uvimbe wa aorta ya tumbo ulisababisha vifo vya karibu 167,000, wengi wao wakiwa wanaume wazee.[6] Hii iliongezeka kutoka karibu 100,000 mwaka wa 1990, iliyopunguka kwa kiasi fulani katika nchi zilizoendelea lakini ya kuongeza mzigo katika nchi zinazoendelea katika watu wanaozeeka.[6] Nchini Marekani, Uvimbe wa aorta ya tumbo ulisababisha vifo kati ya 10,000 na 18,000 mwaka wa 2009.[4]
Marejeleo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 1.15 1.16 1.17 1.18 1.19 1.20 1.21 Kent KC (27 Novemba 2014). "Clinical practice. Abdominal aortic aneurysms". The New England Journal of Medicine. 371 (22): 2101–8. doi:10.1056/NEJMcp1401430. PMID 25427112.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 Upchurch GR, Schaub TA (2006). "Abdominal aortic aneurysm". Am Fam Physician. 73 (7): 1198–204. PMID 16623206.
- ↑ 3.0 3.1 Wittels K (Novemba 2011). "Aortic emergencies". Emergency Medicine Clinics of North America. 29 (4): 789–800, vii. doi:10.1016/j.emc.2011.09.015. PMID 22040707.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 4.2 4.3 "Aortic Aneurysm Fact Sheet". cdc.gov. Julai 22, 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Februari 2015. Iliwekwa mnamo 3 Februari 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 5.0 5.1 5.2 Bunce, Nicholas H.; Ray, Robin; Patel, Hitesh (2020). "30. Cardiology". Katika Feather, Adam; Randall, David; Waterhouse, Mona (whr.). Kumar and Clark's Clinical Medicine (kwa Kiingereza) (tol. la 10th). Elsevier. ku. 1129–1130. ISBN 978-0-7020-7870-5. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-01-23. Iliwekwa mnamo 2022-01-22.
- ↑ 6.0 6.1 6.2 Wei, Linyan; Bu, Xiang; Wang, Xiqiang; Liu, Jing; Ma, Aiqun; Wang, Tingzhong. "Global Burden of Aortic Aneurysm and Attributable Risk Factors from 1990 to 2017". Global Heart. 16 (1): 35. doi:10.5334/gh.920. ISSN 2211-8160. PMID 34040948. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-01-26. Iliwekwa mnamo 2022-01-26.
{{cite journal}}
: CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ Logan, Carolynn M.; Rice, M. Katherine (1987). Logan's Medical and Scientific Abbreviations. Philadelphia: J. B. Lippincott Company. uk. 3. ISBN 978-0-397-54589-6.
- ↑ Spangler R, Van Pham T, Khoujah D, Martinez JP (2014). "Abdominal emergencies in the geriatric patient". International Journal of Emergency Medicine. 7 (1): 43. doi:10.1186/s12245-014-0043-2. PMC 4306086. PMID 25635203.
{{cite journal}}
: CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ LeFevre ML (19 Agosti 2014). "Screening for abdominal aortic aneurysm: U.S. Preventive Services Task Force recommendation statement". Annals of Internal Medicine. 161 (4): 281–90. doi:10.7326/m14-1204. PMID 24957320.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Svensjö, S; Björck, M; Wanhainen, A (Desemba 2014). "Update on screening for abdominal aortic aneurysm: a topical review". European Journal of Vascular and Endovascular Surgery. 48 (6): 659–67. doi:10.1016/j.ejvs.2014.08.029. PMID 25443524.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Thomas DM, Hulten EA, Ellis ST, Anderson DM, Anderson N, McRae F, Malik JA, Villines TC, Slim AM (2014). "Open versus Endovascular Repair of Abdominal Aortic Aneurysm in the Elective and Emergent Setting in a Pooled Population of 37,781 Patients: A Systematic Review and Meta-Analysis". ISRN Cardiology. 2014: 149243. doi:10.1155/2014/149243. PMC 4004021. PMID 25006502.
{{cite journal}}
: CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ Biancari F, Catania A, D'Andrea V (Novemba 2011). "Elective endovascular vs. open repair for abdominal aortic aneurysm in patients aged 80 years and older: systematic review and meta-analysis". European Journal of Vascular and Endovascular Surgery. 42 (5): 571–6. doi:10.1016/j.ejvs.2011.07.011. PMID 21820922.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Paravastu SC, Jayarajasingam R, Cottam R, Palfreyman SJ, Michaels JA, Thomas SM (23 Januari 2014). "Endovascular repair of abdominal aortic aneurysm". The Cochrane Database of Systematic Reviews. 1 (1): CD004178. doi:10.1002/14651858.CD004178.pub2. PMID 24453068.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Ilyas S, Shaida N, Thakor AS, Winterbottom A, Cousins C (Februari 2015). "Endovascular aneurysm repair (EVAR) follow-up imaging: the assessment and treatment of common postoperative complications". Clinical Radiology. 70 (2): 183–196. doi:10.1016/j.crad.2014.09.010. PMID 25443774.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)