Sinkopu
A 1744 oil painting by Pietro Longhi called Fainting | |
ICD-10 | R55. |
---|---|
ICD-9 | 780.2 |
DiseasesDB | 27303 |
MedlinePlus | 003092 |
eMedicine | med/3385 ped/2188 emerg/876 |
MeSH | D013575 |
Sinkopu, ambayo pia hujulikana kama kupoteza fahamu au kuishiwa na pumzi, hufasiliwa kama upotezaji mfupi wa fahamu na nguvu za misuli, unaoanyeshwa kwa mwanzo wa haraka, wa muda mfupi wa upataji tena fahamu. Hutokana na kupungua kwa mtiririko wa katika ubongo kutokana na shikizo la chini la damu. Visababishi vingine vina dalili za onyo kabla ya upoteaji wa fahamu kutendeka. Dalili hizi zinaweza kuwa wepesi wa kichwa, kutokwa na jasho, ngozi iliyokwajuka, kutoona vizuri, kutaka kutapika, kutapika, na kujihisi moto miongoni mwa zingine. Sinkopu inaweza pia kuhusishwa na kipindi kifupi cha mshtuko wa misuli. Mtu asipopoteza fahamu na nguvu za misuli kikamilifu, huitwa kitanguliza sinkopu. Imependekezwa kuwa kitanguliza sinkopu kishughulikiwe kwa njia sawa na sinkopu.[1]
Kisababishi
[hariri | hariri chanzo]Visababishi ni kutoka kwa visivyo hatari hadi vinavyoweza kusababisha kifo Kuna kategoria tatu pana za visababishi: vinavyohusiana na moyo au mshipa wa damu, rifleksi ambayo pia hujulikana kama inayotokana na neva, na hipotensheni ya wima. Masuala yanayohusiana na moyo na mishipa ya damu ndiyo kisababishi cha takribani asilimia 10 na ambacho ndicho hatari sana ilhali inayotokana na neva ndiyo inayotokea sana. Visababishi vinavyotokana na moyo vinaweza kuwa ridhimu isiyo ya kawaida ya moyo, matatizo ya vali za moyo au misuli ya moyo na kufungana kwa mishipa ya damu kutokana na uemboli wa mishipa au uchanguaji wa mshipa wa aota miongoni mwa mengine. Sinkopu inayotokana na neva hutokea mishipa ya damu inapotanuka na upunguaji wa kasi ya mdundo wa moyo isivyofaa. Hii inaweza kutokana na tukio la kuchochea kama vile kutangamana na damu, maumivu au hisia nzito au shughuli maalum kama vile kukojoa, kutapika, au kukohoa. Aina hii ya sinkopu inaweza pia kutokea sehemu kwenye shingo iitwayo sinasi ya karotidi inapofinywa. Aina ya mwisho ya sinkopu hutokana na kupungua kwa shinikizo la damu kutokana na kusimama wima. Hii hutokana na dawa ambazo mtu anatumia lakini pia inaweza kuhusiana na kuishiwa na maji mwilini, kuvuja damu nyingi au maambukizi.[1]
Utambuzi na udhibiti
[hariri | hariri chanzo]Historia ya kiafya, uchunguzi wa mwili, na elektrokadiogramu (EKG) ndizo njia bora zaidi za kutambua kisababishi halisi. EKG ni muhimu kutambua ridhimu isiyo ya kawaida ya moyo, mtiririko duni wa damu kwenye misuli ya moyo, na tatizo linguine la kielektriki kama vile sindromu ndefu ya QT na -a Brugada. Visababishi vinavyohusiana na moyo pia huwa na historia finyu ya dalili za awali. Shinikizo la chini la damu na mdundo wa kasi wa moyo baada ya tukio hilo linaweza kuashiria upotezaji wa damu au kuishiwa na maji, ilhali viwango vya chini vya oksijeni inaweza kuonekana kufuatia tukio kwa walio na uemboli wa mishipa. Vipimo mahususi kama vile vifaa vya kurekodi lupu vya kuweka, kipimo cha kupinda meza au mkando wa sinasi ya karotidi vinaweza kutumiwa kwa visa visivyo wazi. Tomografia ya kompyuta (CT) haihitajiki isipokuwa kuna ila maalum. Visababishi vingine vya dalili sawa vinavyofaa kuzingatiwa vikiwemo tukutiko, kiharusi, konkasheni, kiwango cha chini cha oksijeni kwenye damu, kiwango cha chini cha sukari kwenye damu, usumisho utokanao na dawa na matatizo mengine ya saikiatria miongoni mwa mengine. Matibabu hulingana na kisababishi halisi. Wanaozingatiwa kuwa katika hatari kubwa baada ya utambuzi wanaweza kulazwa hospitalini kwa ufuatiliaji wa moyo zaidi.[1]
Epidemiolojia na prognosisi
[hariri | hariri chanzo]Sinkopu huathiri takribani watu watatu hadi sita kwa kila watu elfu moja kila mwaka.[1] Hutokea sana kwa wazee na wanawake. Ndiyo sababu ya asilimia moja hadi tatu ya safari kwa vitengo vya dharura na kulazwa hospitalini. Hadi nusu ya wanawake zaidi ya umri wa miaka 80 na thuluthi moja ya wanafunzi wa udaktari huelezea angalau tukio moja maishani mwao.[2] Kwa wote walio na sinkopu, takribani asilimia 4 hufariki kwa siku 30 zinazofuata.[1] Hatari ya matokeo mabaya, hata hivyo, hulingana na kisababishi halisi.[3]
Marejeleo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 Peeters, SY; Hoek, AE; Mollink, SM; Huff, JS (Aprili 2014). "Syncope: risk stratification and clinical decision making". Emergency medicine practice. 16 (4): 1–22, quiz 22-3. PMID 25105200.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kenny, RA; Bhangu, J; King-Kallimanis, BL (2013). "Epidemiology of syncope/collapse in younger and older Western patient populations". Progress in cardiovascular diseases. 55 (4): 357–63. PMID 23472771.
- ↑ Ruwald, MH (Agosti 2013). "Epidemiological studies on syncope--a register based approach". Danish medical journal. 60 (8): B4702. PMID 24063058.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)