Usunga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Usunga ni kata ya Wilaya ya Sikonge katika Mkoa wa Tabora, Tanzania, yenye postikodi namba 45316.

Katika kata hiyo kuna vijiji vinne navyo ni: Usunga, Urafiki, Isanjandugu na Mwanamkata.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa 10,564 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,140 waishio humo.[2]

Kata hiyo ina mchanganyiko wa makabila ya Wasukuma na Wanyamwezi.

Kuna shule ya sekondari moja, ambayo ni Usunga secondary school, zahanati moja, vyama vya msingi vitatu vya wakulima wa tumbaku, taasisi za dini, timu za mpira wa miguu n.k.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Sikonge - Mkoa wa Tabora - Tanzania

Chabutwa | Igigwa | Ipole | Kiloleli | Kiloli | Kilumbi | Kipanga | Kipili | Kisanga | Kitunda | Misheni | Mkolye | Mole | Mpombwe | Ngoywa | Nyahua | Pangale | Sikonge | Tutuo | Usunga


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tabora bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Usunga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.