Nenda kwa yaliyomo

Uruguay (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Uruguay River)
Mto wa Uruguay
Chanzo milima ya Serra Geral (Brazil)
Mdomo Rio Plata
Nchi Brazil, Argentina, Uruguay
Urefu 1,790 km
Kimo cha chanzo takriban 1,800 m
Mkondo 4,622 m³/s
Eneo la beseni 370,000 km²
Miji mikubwa kando lake Concepción del Uruguay, Paysandu,
Mto Uruguay

Uruguay ni mto wa Amerika Kusini. Pamoja na mto Parana unaishia katika Rio de la Plata. Jina Uruguay linamaanisha "mto wa ndege ya rangi nyingi".

Chanzo chake ni Brazil ya Kusini kwenye jimbo la Santa Catarina. Mwanzo wake ni mpaka kati ya majimbo ya Santa Catarina na Rio Grande do Sul ndani ya Brazil; baada ya mpaka kati ya Brazil na Argentina, halafu kati ya Argentina na Uruguay.

Jina la nchi ya Uruguay limetokana na mto huo na ni "Jamhuri upande wa magharibi ya mto Uruguay".

Meli haziingii sana ndani ya Uruguay kutokana na maporomoko yake.

Ramani ya njia ya mto Uruguay

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Uruguay (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.