Nenda kwa yaliyomo

Umoja wa Kizalendo kwa Ukombozi wa Vietnam Kusini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Vietkong

Umoja wa Kizalendo kwa Ukombozi wa Vietnam Kusini (pia: Vietkong, NLF) ilikuwa harakati ya kijeshi chini ya uongozi wa wakomunisti katika Vietnam Kusini iliyopinga serikali ya Vietnam Kusini pamoja na wasaidizi wake Wamarekani kuanzia 1960 hadi 1975.

Ilijulikana kimataifa mara nyingi kwa kufupi cha "Vietkong" au kifupi cha Kiingereza cha "NLF" (National Liberation Front).

Vietkong ilianzishwa kwa amri wa chama cha kikomunisti cha Vietnam Kaskazini mwaka 1960 kwa lengo la kuchukua utawala wa kusini ya Vietnam. Harakati mpya ulijengwa juu ya ushirikiano wa mabaki ya wapinzani wa kale dhidi ya ukoloni wa Ufaransa ambao hawakuridhiki na serikali ya Vietnam Kusini pamoja na maafisa kutoka kaskazini. Msingi huu uliwapa Vietkong vituo vingi kote Vietnam Kusini ambako walikuwa na wasaidizi na wanachama. Lakini uongozi ulikuwa mkononi mwa Vietnam Kaskazini na wakati wa vita ya Vietnam idadi ya wanajeshi kutoka kaskazini iliongezeka mfululizo.

Mwishoni vikundi wa askari wa kusini walikuwa sehemu ndogo tu pamoja na vikosi vya kijeshi kutoka Vietnam Kaskazini ingawa kwa jina mapambano yote yalitekelezwa na Vietkong.

Vietkong ilipigania vita ya msituni na kusababisha jeshi la Marekani kuondoka Vietnam Kusini hadi 1975.