Nenda kwa yaliyomo

Ulipuaji wa makao makuu ya serikali ya Algeria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ulipuaji wa makao makuu ya serikali ya Algeria yalitokea mnamo tarehe 11 Aprili mwaka 2007 wakati mabomu mawili ya kujitoa mhanga yalipolipuka katika mji mkuu wa Algeria, Algiers.

Makao makuu ya Waziri Mkuu wa Algeria yalishambuliwa na mlipuko mkubwa uliosababisha vifo na majeruhi wengi na ulisikika kilomita 10 kutoka eneo la tukio. Mlipuko mwingine ulilenga kituo cha polisi katika kitongoji cha mashariki mwa mji, karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Houari Boumediene.

Al-Qaeda walidai kuhusika na mabomu hayo baada ya shambulizi kutokea.[1]

  1. "Al Qaida claims Algeria blasts", Al Jazeera, 12 April 2007. Retrieved on 3 June 2008. Archived from the original on 1 April 2008. 
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ulipuaji wa makao makuu ya serikali ya Algeria kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.