Ulindwanoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ulindwanoni ni kijiji cha kata ya Ufukutwa (msimbo wa posta 45719) kwenye Wilaya ya Kaliua (Mkoa wa Tabora). Kipo kilometa 5 magharibi ya Kaliua mjini. Kina wakazi wapatao 4,126 kwa sensa ya mwaka 2012.

Ndicho kijiji alichozaliwa mbunge wa Urambo Magharibi Juma Kapuya.

Wakazi wa eneo hili ni jamii za wakulima na wafugaji. Zao kuu la biashara linalolimwa ni tumbaku.