Ulemavu katika Afrika Mashariki
Ulemavu katika Afrika Mashariki ni suala tofauti kabisa na dhana za watu wanaotoka nje ya bara. Watu wengi wanadhani kwamba nchi za Afrika Mashariki hazielewi ulemavu na kwamba watu wengi wa Afrika Mashariki wanabeba dhana ya kienyeji kuwa watu walio na ulemavu wamezaliwa kwa sababu familia zao walifanya kitendo kibaya sana au uchawi, ndio uliosababisha mtu kuwa na ulemavu. Lakini, iwe Magharibi au Mashariki, Kaskazini au Kusini, kuna walemavu katika kila sehemu ya dunia, na katika kila nchi na utamaduni walifanya makosa wakati wa kujaribu kuelewa na kusaidia walemavu.
Katika Afrika Mashariki, watu waliokuwa na ulemavu walionwa kama matendo ya adhabu kutoka kwa Mungu.
Upofu umefahamika katika utamaduni wa Afrika Mashariki kwa muda mrefu. Nahau za Kiswahili zinatupa mafunzo kuhusu maisha ya mtu aliye kipofu. Nahau kama “Kipofu hamwelekezi kipofu mwingine kwa mwenge”.[1] Nahau hii ni inafanana na nahau ya Kiingereza inayosema “Kipofu akiongoza kipofu basi wataanguka katika shimo”.[1]
Katika siku za ukoloni, mfumo wa uchumi wa nchi za Afrika Mashariki ulikuwa ukiongozwa na serikali za Ujerumani na Uingereza. Kabla ya ukoloni, watu wengi walilima mashamba binafsi. Wakati wa ukoloni, watu wengi waliondoka nyumbani kwao ili kufanya kazi katika miji au mashamba makubwa[2]. Watu wenye ulewavu hawakuwa na nguvu ya kutosha kufanya kazi katika viwanda au mashamba kwa hiyo wakati watu wengi waliondoka, watu walewavu walikaa peke yao. Kulikuwa na fursa chache siku hizo kwa watu wenye ulemavu kuenda shuleni katika Afrika Mashariki. Lakini, katika mwaka wa elfu moja mia tisa arobaini na sita, Shule ya Vipofu ya Thika ilifunguliwa[2]. Shule hii ilianzishwa na Jeshi la Wokovu na iliwapa wanafunzi vipofu fursa ya kusoma kwa mara kwanza katika Kenya. Katika mwaka wa 1963, shule iliyoitwa Shule ya Wasichana vipofu ya Irente ilianza kuwapa mafunzo ya taaluma wasichana wenye ulemavu.
Hivi sasa, watu wengi wanaamini kwamba serikali za Afrika Mashariki zinafaa kufanya juhudi zaidi kuwashughulikia watu walio na ulemavu. Katika mwaka wa 2006, Umoja wa Mataifa (United Nations) waliongoza njia kuhifadhi usawa wa watu walemavu katika macho ya serikali za Afrika Mashariki. Vyama vya watu walemavu vimeanza kuwa na sauti kwa mfano katika siasa. Vyama hivi vina mwito. Mwito wao ni “Hamna kitu kutuhusu sisi bila sisi”, au “Nothing about us without us” kwa Kiingereza.[3] Hata hivyo, vyama vingi havina watu wenye ulemavu wa ubongo. Vingi vina watu wenye ulemavu wa mwili tu. Katika wakati wa usoni, ni muhimu kwa wanasiasa kuunda sheria zinazowashirikisha watu walio na ulemavu wa mwili na ubongo pia.[4] Chini ya sheria za Jumuiya ya Afrika Mashariki (East African Community), wanachama wakiwa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Sudan Kusini na Burundi, kama nchi moja haikubaliani na nchi nyingine[5], basi kila nchi haiwezi kukubaliana na Umoja wa Mataifa. Burundi ndiyo nchi pekee katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo haijakubali kupitisha mpango wa Umoja wa Mataifa.[4]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "Kisanji, Joseph. Attitudes and Beliefs about Disability in Tanzania. University of Manchester, english.aifo.it/disability/documents/innovations/5kisanji.pdf" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-12-22. Iliwekwa mnamo 2019-07-26.
- ↑ 2.0 2.1 Gebrekidan, Fikru Negash. “Disability Rights Activism in Kenya, 1959-1964: History from Below.” African Studies Review, vol. 55, no. 3, 2012, pp. 103–122. JSTOR, www.jstor.org/stable/43904850.
- ↑ Hoffmann, Corina. “‘Disability-Rights-Movement in East Africa: The Role and Impact of Self-Representation of Persons with Disabilities on National, Transnational and Regional Level.’” ECPR, Max Planck Institute for Social Law and Social Policy, 15 Apr. 2014, ecpr.eu/Filestore/PaperProposal/60b58c73-a93a-44ab-92db-0fb846577fd8.pdf.
- ↑ 4.0 4.1 Ndetei, David M, et al. “Kenya's Mental Health Law.” BJPsych International, The Royal College of Psychiatrists, 1 Nov. 2017, www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5663024/.
- ↑ Secretariat, EAC. “EAC Policy on Persons With Disabilities.” MEAC, East African Community, Mar. 2012, meac.go.ke/wp-content/uploads/2017/03/adopted_eac_disability_policy_march_2012.pdf.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ulemavu katika Afrika Mashariki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |