Ukame wa Eire

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ukame Mkubwa au Njaa Kubwa (kwa Kieire: An Gorta Mór au An Drochshaol) ni jina la kipindi cha ukame nchini Eire kati ya miaka 1845 na 1849. Nje ya Eire, mara nyingi waliita Irish Potato Famine yaani Ukame wa Mbatata Eire. Ukame huo ulisababishwa na mabaka-baka. Mabakabaka ilikuwa ugonjwa uliyoharibu viazi mbatata vya nchini Eire kwa haraka sana.

Viazi mbatata ilikuwa chakula kikubwa kwa nchi ya Eire kwa kipindi hicho. Athali za ukame huo zilikuja kwisha mnamo mwaka wa 1851. Mengi yaliyotokea hayakuwahi kujuilikana kwa kipindi hicho.

Inasadikika kuwa takriban watu 500,000 na zaidi ya milioni moja walipoteza maisha kwa njaa au magonjwa katika miaka hiyo mitatu, kuanzia 1846 hadi 1849. Mamilion ya wengine wakaja kuwa wakimbizi kwasababu ya ukame. Waliondoka Eire na kuhamia Britania, Marekani, Kanada, na Australia.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukame wa Eire kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.