Nenda kwa yaliyomo

Ugonjwa wa mshtuko wa sumu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ugonjwa wa mshtuko wa sumu
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuUgonjwa wa kuambukizwa
Dalilihoma, upele, kuchibuka ngozi, shinikizo la chini la damu[1]
Muda wa kawaida wa kuanza kwakeHuanza kwa ghafla na haraka sana[1]
VisababishiStreptococcus pyogenes, Staphylococcus aureus, nyingine[1][2]
Sababu za hatariTamponi zenye uwezo mkubwa sana wa kufyonza damu, vidonda vya ngozi miongoni mwa watoto wachanga[1]
Njia ya kuitambua hali hiiKulingana na dalili[1]
Utambuzi tofautiMshtuko wa septiki, Ugonjwa wa Kawasaki, Maradhi ya Stevens-Johnson, maradhi yasababishayo vipele ngozini[3]
MatibabuMatumizi ya Antibiotiki, upasuaji na uondoaji wa usaha wowote kwenye tishu, uwekaji wa immuniglobulini kwenye mishipa[1]
Utabiri wa kutokea kwakeHatari ya kifo kutokea: ~asilimia 50% kwa (streptococcal), ~asilimia 5% kwa (staphylococcal)[1]
Idadi ya utokeaji wakewatu 3 kati ya watu 100,000 kwa mwaka (nchi zilizokua kimaendeleo)[1]

Ugonjwa wa mshtuko wa sumu (kwa Kiingereza: Toxic shock syndrome, TSS) ni hali inayosababishwa na sumu za bakteria.[1] Dalili zinaweza kujumuisha homa, upele, kuchibuka kwa ngozi na shinikizo la chini la damu.[1] Kunaweza pia kuwa na dalili zinazohusiana na maambukizi maalum yaliyopo mwilini kama vile ugonjwa wa matiti (mastitis), ugonjwa wa mifupa (osteomyelitis), ugonjwa wa kuoza kwa tishu za mwili (netrotising fasciitis) au nimonia.[1]

Ugonjwa wa TSS kwa kawaida husababishwa na bakteria wa aina ya Streptococcus pyogenes au Staphylococcus aureus, ingawa bakteria wengine wanaweza pia kuhusika.[1][2] Ugonjwa wa mshtuko wa sumu wa Streptococcal wakati mwingine unajulikana kama ugonjwa unaofanana na mshtuko wa sumu (TSLS).[1] Michakato ya msingi iliyopo huhusisha uzalishaji wa antijeni kuu (superantigens) wakati wa maambukizi vamizi ya streptococcus au maambukizi ya sehemu mahususi ya mwili ya staphylococcus.[1] Sababu za hatari zinazoweza kuongeza maambukizi ya aina ya staphylococcal ni pamoja na matumizi ya tamponi zenye uwezo mkubwa sana wa kufyonza damu na vidonda vya ngozi kwa watoto wadogo.[1] Kwa kawaida, utambuzi wa ugonjwa huo hutegemea dalili.[1]

Matibabu yake yanajumuisha uwekwaji wa viowevu kwenye mishipa, matumizi ya antibiotiki, upasuaji na uondoaji wa usaha wowote kwenye tishu na ikiwezekana uwekwaji wa immunoglobulini kwenye mishipa.[1][4] Haja ya kuondolewa kwa haraka kwa tishu zilizoambukizwa kupitia upasuaji kwa wale waliougua kutokana maambukizi ya streptococcal, ingawa inapendekezwa sana, haina ushahidi wa kutosha wa kuiunga mkono.[1] Watu wengine hupendekeza kuchelewesha mchakato wa uondoaji wa tishu zilizoambukizwa kwa njia ya upasuaji.[1] Hatari ya jumla ya kifo kutokea kutokana na ugonjwa wa streptococcal ni takribani asilimia 50%, na asilimia 5% kutokana na ugonjwa wa staphylococcal.[1] Kifo kinaweza kutokea ndani ya siku 2.[1]

Nchini Marekani ugonjwa wa streptococcal TSS hutokea kwa takriban watu 3 kati ya watu 100,000 kwa mwaka na ugonjwa wa staphylococcal TSS kwa takriban 0.5 kati ya watu 100,000 kwa mwaka.[1] Ugonjwa huo hutokea zaidi zaidi katika nchi zinazoendelea kukua.[1] Ugonjwa huu ulielezewa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1927.[1] Kwa sababu ya kuhusishwa kwake na tamponi zenye uwezo mkubwa sana wa kufyonza damu, bidhaa hizi ziliacha kuuzwa.[1]

  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 1.15 1.16 1.17 1.18 1.19 1.20 1.21 1.22 1.23 1.24 Low, DE (Julai 2013). "Toxic shock syndrome: major advances in pathogenesis, but not treatment". Critical Care Clinics. 29 (3): 651–75. doi:10.1016/j.ccc.2013.03.012. PMID 23830657.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 Gottlieb, Michael; Long, Brit; Koyfman, Alex (Juni 2018). "The Evaluation and Management of Toxic Shock Syndrome in the Emergency Department: A Review of the Literature". The Journal of Emergency Medicine. 54 (6): 807–814. doi:10.1016/j.jemermed.2017.12.048. PMID 29366615.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Ferri, Fred F. (2010). Ferri's differential diagnosis : a practical guide to the differential diagnosis of symptoms, signs, and clinical disorders (tol. la 2nd). Philadelphia: Elsevier/Mosby. uk. Chapter T. ISBN 978-0323076999.
  4. Wilkins, Amanda L.; Steer, Andrew C.; Smeesters, Pierre R.; Curtis, Nigel (2017). "Toxic shock syndrome – the seven Rs of management and treatment". Journal of Infection (kwa Kiingereza). 74: S147–S152. doi:10.1016/S0163-4453(17)30206-2. PMID 28646955.