Ugonjwa na mtu mgumu
| Ugonjwa na mtu mgumu | |
|---|---|
| Mwainisho na taarifa za nje | |
| Kundi Maalumu | Nurologia |
| Dalili | Misuli ngumu, mikazo ya ghafla ya misulu, maumivu[1][2] |
| Muda wa kawaida wa kuanza kwake | 20 hadi 60[2] |
| Muda | Kuzidi kuzorota kwa kasi[2] |
| Visababishi | Haijulikani, kingamwili kuzalishwa dhidi ya vitu asili vya mwilini [1] |
| Njia ya kuitambua hali hii | Kulingana na dalili na kuungwa mkono na vipimo vya damu na elektromiografia[2] |
| Utambuzi tofauti | Parkinsons, multiple sclerosis, fibromyalgia, psychosomatic illness, anxiety[1] |
| Matibabu | Diazepam, baclofen, gabapentin, intravenous immunoglobulin[1][3] |
| Utabiri wa kutokea kwake | Mara nyingi huwa mbaya sana [3][4] |
| Idadi ya utokeaji wake | Nadra[5] |
Ugonjwa na mtu mgumu (kwa Kiingereza: Stiff-person syndrome) ni ugonjwa wa neurolojia unaojulikana kwa misuli migumu na mikazo ya ghafla ya misuli ambayo huwa mibaya zaidi muda unapozidi kusonga.[5][1] Ugonjwa huu unaathiri kimsingi kiwiliwili, mikono na miguu.[1] Mikazo ya ghafla ya misuli inaweza kuchochewa na sauti, mguso, au hisia.[5] Matatizo yake yanaweza kujumuisha mkao mbaya, kuvunjika kwa mfupa, maumivu makali mno ya muda mrefu, na kuanguka mara kwa mara.[5][1][3]
Katika hali nyingi, sababu zake hazijulikani, ingawa utaratibu wa ugonjwa unaosababishwa na kingamwili kuzalishwa dhidi ya vitu asili vilivyopo mwilini unaaminika kuhusika.[1] Kesi nyingi zinahusishwa na hali zingine za kingamwili, kama vile kisukari cha aina ya 1.[4] Mara nyingi hutokea kama ugonjwa wa paraneoplastiki.[3][4] Utambuzi wake mara nyingi hufanyika kwa kupata viwango vya juu sana vya kingamwili hadi kuwepo kwa asidi ya glutamic decarboxylase (GAD) katika damu au maji ya uti wa ubongo.[1][3] Electromiografia inaweza pia kuwa muhimu.[5]
Dalili zake zinaweza kutibiwa kwa dawa kama vile diazepam, baclofen, au gabapentin.[1] Imunoglobulini ya mishipa au kuondoa maji ya damu kutoka mwilini kwa kutoa damu, kuitenganisha maji ya damu na seli, na kurudisha seli kwenye mkondo wa damu pia inaweza kusaidia.[1][3] Kwa ujumla husababisha ubora duni wa maisha, na unyogovu au wasiwasi mara nyingi hutokea kama matokeo yake.[3][4] Husababisha matarajio ya maisha yaliyopunguka.[4]
Ugonjwa wa mtu mgumu ni nadra, hutokea kwa karibu mtu mmoja kati ya milioni.[3] Huanza mara nyingi kati ya umri wa miaka 20 na 60, ingawa inaweza kutokea kwa watoto kwa njia isiyo ya kawaida.[2] Wanawake huathiriwa mara mbili zaidi kuliko wanaume.[1] Hali hiyo ilielezewa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1956 na Frederick Moersch na Henry Woltman.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 "Stiff-Person Syndrome | National Institute of Neurological Disorders and Stroke". www.ninds.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Desemba 2022. Iliwekwa mnamo 9 Desemba 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 4 5 6 Muranova, A; Shanina, E (Januari 2022). "Stiff Person Syndrome". PMID 34424651.
{{cite journal}}: Cite journal requires|journal=(help)CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 4 5 6 7 8 Ortiz, JF; Ghani, MR; Morillo Cox, Á; Tambo, W; Bashir, F; Wirth, M; Moya, G (9 Desemba 2020). "Stiff-Person Syndrome: A Treatment Update and New Directions". Cureus. 12 (12): e11995. doi:10.7759/cureus.11995. PMID 33437550.
{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unflagged free DOI (link) - 1 2 3 4 5 Hadavi, S; Noyce, AJ; Leslie, RD; Giovannoni, G (Oktoba 2011). "Stiff person syndrome". Practical neurology. 11 (5): 272–82. doi:10.1136/practneurol-2011-000071. PMID 21921002.
{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 4 5 "Stiff person syndrome - About the Disease - Genetic and Rare Diseases Information Center". rarediseases.info.nih.gov (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Novemba 2022. Iliwekwa mnamo 9 Desemba 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)