Uchina Bara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sehemu iliwekwa unjano ni sehemu ya Uchina Bara.

Uchina Bara ni sehemu ya Uchina bila kujumlisha Jamhuri ya China inayomiliki Taiwan, Kinmen, Matsu, na Pescadores. Hii pia inatoa sehemu ya Hong Kong na Macau.

Wakati wa Nasaba ya Qing, sehemu yote ya Uchina Bara, Hong Kong, Macau, Taiwan, Kinmen, Matsu, Pescadores, na Mongolia ilikuwa sehemu ya Dola la Kichina. Taiwan, Hong Kong, na Macau yalitolewa kwa wageni kwa muda kwa miaka kadhaa (Taiwan walipewa Wajapani, Hong Kong walipewa Waingereza, na Macau walipewa Wareno).

Mwishoni mwa Dola la Qing, China ikawa Kuomintang China (Jamhuri ya China) na ikairudisha Taiwan mikononi mwake mnamo mwaka wa 1945. Baadaye ukomunisti (Jamhuri ya Watu wa China) ikachukua sehemu kubwa ya China, na Kuomintang wakabaki na Taiwan, Kinmen, Matsu, na Pescadores. Mongolia baadaye ikawa nchi huru.

Tangu hapo, Uchina ya Kikomunist ikawa imeingiza baadhi ya sehemu za (uchina bara) na baadhi ya vijisiwa ambavyo viliathiriwa na idadi kuwa ya wakomunisti (Hainan). Mkoa huu ni sehemu ya Uchina Bara.

Baadaye Hong Kong na Macau zikarudi mikononi mwa serikali ya China, lakini kuna kipindi hujifikiria kuwa wao kama sio wamoja wa sehemu ya Uchina Bara.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

  • Learn Chinese What is Mandarin? People of Mainland China speak mandarin Chinese.
Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Uchina Bara kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.