Uche Okeke
Christopher Uchefuna Okeke (anajulikana pia kama Uche Okeke; 30 Aprili 1933 - 5 Januari 2016), alikuwa mchoraji, mchongaji, na mwalimu. Okeke alikuwa mwananadharia wa sanaa za urembo, aliyejikita sana Nigeria.
Historia ya Awali
[hariri | hariri chanzo]Christopher Uchefuna Okeke alizaliwa tarehe 30 Aprili 1933 mjini Nimo,[1] katika serikali ya Njikoka Local Government Area katika jimbo la Anambra State, eneo la kusini-mashariki mwa Nigeria, akiwa mwana wa Isaac Okonkwo Okeke na Monica Mgboye Okeke (née Okoye).
Kati ya mwaka 1940 na 1953, alisoma katika Shule ya Msingi ya St. Peter Claver, Kafanchan, Metropolitan College, Onitsha, na Bishop Shanahan College, Orlu, Nigeria. Wakati huo, tayari alionyesha shauku kubwa kwa uchoraji na kupaka rangi.
Kabla ya kuingizwa kusoma Sanaa za Picha katika chuoc cha Nigerian College of Arts, Science and Technology (NCAST), sasa kinaitwa Ahmadu Bello University, mjini Zaria, Okeke tayari alikuwa amejitokeza katika tasnia ya sanaa. Alionyesha kazi zake za taxidermy katika mkutano wa Field Society kwenye nyumba ya makumbushi liitwalo Jos Museum, kushiriki katika maandalizi na maonyesho ya michoro na uchoraji wa Nigeria akiwa na Bernard Fagg kama mkaguzi, na pia alikuwa na maonyesho ya kibinafsi ya michoro na uchoraji , mjini Jos na Kaduna akiwa na Sir Ahmadu Bello kama mgeni rasmi.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ [(https://www.vanguardngr.com/2016/02/uche-okeke-1933-2016/) "Uche Okeke (1933-2016)"]. Vanguard News (kwa American English). 2016-02-06. Iliwekwa mnamo 2022-03-05.
{{cite web}}: Check|url=value (help) - ↑ Bernice M. Kelly, "Uche Okeke," in Nigerian Artists, A Who's Who & Bibliography, ed. Janet L. Stanley (Washington DC, 1993), 361-368.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uche Okeke kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |