Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 2016

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka 2016 ulikuwa wa 58 katika historia ya Marekani. Ulifanywa Jumanne tarehe 8 Novemba.

Upande wa "Republican Party", mgombea Donald Trump (pamoja na kaimu wake Mike Pence) alimshinda mgombea wa "Democratic Party" Hillary Clinton (pamoja na kaimu wake Tim Kaine).

Matokeo[hariri | hariri chanzo]

Wachaguzi wakuu walipiga kura tarehe 19 Desemba na kuthibitisha nafasi ya Trump kama Rais wa Marekani kwa miaka 2017-2020. Trump alipata wapiga kura 304, na Clinton 227, wakati wachaguzi wakuu wengine saba walikuwa upande wa watu wasiogombea.