Nenda kwa yaliyomo

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 2012

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 2012 ulikuwa wa 57 katika historia ya Marekani. Ulifanyika siku ya Jumanne tarehe 6 Novemba 2012. Upande wa "Democratic Party", Rais Barack Obama (pamoja na kaimu wake Joe Biden) alimshinda mgombea wa "Republican Party" Mitt Romney (pamoja na kaimu wake Paul Ryan). Ushindi wake (Barack Obama), unatokana na kushinda majimbo yaliyokuwa na ushindani mkubwa ya Ohio, Florida, na Iowa. Matokeo ya uchaguzi huo yalitangazwa rasmi siku ya Jumatano 7 Novemba. [1]

Obama akapata kura 332, na Romney 206. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.

  1. Austin, Sharon Wright; King, Danielle, "President Barack Obama and Racial Politics", The Barack Obama Presidency, Palgrave Macmillan, ISBN 978-0-230-37045-6, iliwekwa mnamo 2024-11-05