Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1976

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1976 ulikuwa wa 48 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 4 Novemba. Upande wa "Democratic Party", mgombea Jimmy Carter (pamoja na kaimu wake Walter Mondale) alimshinda mgombea wa "Republican Party", Rais Gerald Ford (pamoja na kaimu wake Bob Dole).

Matokeo[hariri | hariri chanzo]

Carter akapata kura 279, na Ford 240 wakati mchaguzi mmoja kutoka Washington alimpigia kura Ronald Reagan badala ya Ford. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.