Walter Mondale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Walter Mondale, Kaimu Rais wa Marekani

Walter Frederick "Fritz" Mondale (5 Januari 1928 - 19 Aprili 2021) alikuwa mwanasiasa wa Marekani akiwa mwanachama wa Chama cha Kidemokrasia.

Kuanzia mwaka wa 1964 hadi 1976 alikuwa mbunge wa Senati ya Marekani akiwakilisha jimbo la Minnesota. Halafu alikuwa Kaimu Rais wa Marekani chini ya Rais Jimmy Carter kuanzia mwaka wa 1977 hadi 1981. Mwaka wa 1984 aligombea urais yeye mwenyewe lakini akashindwa na Rais Ronald Reagan.

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Walter Frederick Mondale alizaliwa Januari 5, 1928, katika mji wa Minnesota,[1] wazazi wake walikuwa ni Theodore Sigvaard Mondale, na mama yake akiwa ni Claribel Hope (née Cowan), aliekuwa mwalimu wa muziki .[2][3][4] Mondale pia ana kaka ambao ni Clarence alikuja kujulikana kama Pete pamoja na Wiliam anaejulikana kama Mort, baba zao walihamia kutokea nchini Norwei,[5] Mondale alisoma katika chuo cha Macalester College kwa muda wa miaka miwili kabla ya kuhamia chuo kikuu cha University of Minnesota, na kupata shahada ya sanaa na astashada ya sayansi kaitka siasa mnamo mwaka 1951.[6] baaya ya Mondale kushindwa kujiandikisha katika chuo cha sheria aliamua kujiunga na jeshi mwaka huo huo wa 1951 muda mfupi baada ya kuwa amehitimu masomo yake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. MONDALE, Walter Frederick.
  2. American President: Walter Mondale. Millercenter.org. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-07-04. Iliwekwa mnamo 2021-04-22.
  3. "Walter Mondale". Encyclopædia Britannica. http://www.britannica.com/EBchecked/topic/389066/Walter-Mondale. Retrieved July 20, 2010.
  4. Walter F. Mondale, 42nd Vice President (1977–1981). U.S. Senate.
  5. Jimmy Carter. American Experience. PBS. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-09-12. Iliwekwa mnamo 2021-04-22.
  6. Mondale, Walter Frederick, (1928 – ). Biographical Directory of the United States Congress.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Walter Mondale kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.