Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1916
Mandhari
Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1916 ulikuwa wa 33 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 7 Novemba. Upande wa "Democratic Party", Rais Woodrow Wilson (pamoja na kaimu wake Thomas Marshall) alimshinda mgombea wa "Republican Party" Charles Hughes (pamoja na kaimu wake Charles Fairbanks).
Matokeo
[hariri | hariri chanzo]Wilson akapata kura 277, na Hughes 254. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |